Na Amini Nyaungo
Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Ipembe Mkoani Singida leo imefanya uchaguzi ili kuziba nafasi mbalimbali za uongozi ambazo zilikuwa wazi.
Katika nafasi hizo ni pamoja na Mwenyekiti wa Kata ya Ipembe, Katibu Itikadi Siasa na Uenezi , Mjumbe Mkutano Mkuu Wilaya pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu Kata ya Ipembe.
Baada ya kufanyika kwa uchaguzi huo huru ulifanyika Ukumbi wa Moscow Mwenyekiti aliyetangazwa na msimamizi wa kura ni Anti Debora, huku Katibu wa Itikadi Siasa na Uenezi akichaguliwa Miraji Hamisi na nafasi nyingine.
Baada ya uchaguzi huo Mwenyekiti wa Kata ya Ipembe aliyechaguliwa Anti Debora ameomba ushirikiano kwa wanachama wote wa kata hiyo na kuahidi kufanyakazi kwa moyo wake wote.
"Naomba ushirikiano wenu ili tufike salama naahidi ushirikiano kutoka kwangu,"Debora
Kwa upande wa Miraji Hamisi ambaye kwa sasa ndiye Katibu wa Itikadi , Siasa na Uenezi Kata ya Ipembe amewaambia wanachama wote wamtume kadri sawezavyo ili kazi ziendelee na kuahidi kujitoa kwa hali na mali.
"Naomba mnitume mie nipo kwa ajili yenu, nitajitoa kadri niwezavyo ili chama kiendeles kuwa bora kila siku,"Miraji.
Uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki kwa wajumbe wote waliohudhuria baada ya uchaguzi waliopata kura kidogo ambao wameshindwa wamekiri kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki na watawapa ushirikiano waliochaguliwa.
Mwisho.



Post a Comment