Baada ya kutoa mashuka Hanje amewaomba wananchi waendelee kumuamini Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada mbalimbali anazozifanya kuwakomboa wananachi wake katika nyanja mbalimbali, kwa kile ambacho amekifanya katika kata hiyo moja na matunda yake pamoja na maono yake kama Mbunge kuwasaidia wananchi wake.
"Tuendelee kumuunga mkono Rais Samia kwani anafanya vizuri katika kuliendesha taifa letu, "Hanje
Hanje amesema kuwa atazidi kuwatembelea wananchi katika jimbo hilo na kama ambayo ilivyo sasa tayari ziara yake inaendelea kwa ajili ya kubadilishana mawazo na wakazi wa jimbo hilo pamoja na kutoa kwa kile ambacho amejaaliwa kwa ajili ya kuwasaidia.
Aidha ametumia fursa hiyo kuhubiri juu ya amani ya nchi amewataka Wananchi wa Singida wasiharibu amani iliyopo kwabi ikipotea hakuna wakuweza kuirudisha, akitoa mifano kuwa nchi nyingi duniani zinaitazama Tanzania kama mfano mzuri wa kuigwa kwa amani.
" Tuendelee kuilinda na kuitunza amani ya nchi yetu, hii ni tunu tuliyopewa na Mungu tuilinde,"ameongeza
Mwisho
Post a Comment