WIZI WA MIUNDOMBINU YA TANESCO WAHATARISHA MAISHA YA KIJANA MANYONI

 


Na Amini Nyaungo



Vijana wameombwa kujitafutia kipato kwa njia ya halali ili kuepusha madhara yanayo tokana na wizi kama ambavyo alivyofanya Rajabu Jumanne Mkazi wa kijiji cha Njilii Halmashauri ya Itigi Wilaya ya Manyoni aliyepigwa na shoti ya umeme na kupoteza nguvu ya kutembea baada ya kuiba baadhi ya vifaa vya Transfoma ya Tanesco.


Hayo ameyasema leo Emanuel Soghweda, Diwani wa Kata ya Aghod Halmashauri ya Itigi wilaya ya Manyoni Mkoani Singida baada ya Chamber Media kufika Kijiji cha Njilii ambapo Rajabu Jumanne alikuwa anaiba miundombinu ya Tanesco majira ya saa nane usiku ndipo akapigwa na shoti ya umeme na kupoteza fahamu hivyo Diwani huyo amewaomba watumie nguvu zao katika kutafuta vilivyo vya halali.


" Nimepata taarifa hii kutoka kwa wananchi nimefika hapa namuona kijana huyu aliyekuwa anaiba miundombinu ya umeme na kupigwa shoti hivyo niwaase vijana watumie nguvu zao kutafuta vilivyo vya halali,"Soghweda


Katika hatua nyingine diwani huyo amesema kuwa tukio limetokea saa nane usiku kwa mujibu wa mahojiano na mhalifu ambapo pia amethibitisha kuwa amezoea kuiba. 


Mhandisi wa Tanesco Wilaya ya Manyoni Vicent Temba amesema kuwa watu wasiokuwa na nia njema wameiba miundombinu ya Tanesco ambapo wamefanya uharibifu ambao ni mkubwa, huku zaidi ya Transfoma tatu zimeharibiwa na wahalifu kwa kuiba baadhi ya miundombinu yake ikiwemo waya wa kopa.


Aidha kwa upande wake  Sudi Rashid Mjomba wa Mjomba mhalifu huyo amewaomba vijana kujituma kawaida ili kuepuka madhara kama hayo yaliyotokea kwa mjomba wake.


" Niwaombe vijana wasiibie watafute maisha kwa njia ya halali ili wasipatwe kama yaliyotokea kwa ndugu yangu huyu," Sudi

Deus Migulu ni mwanakijiji wa Njilii amesema kuwa tukio hilo limemfundisha mengi moja wapo ni kuacha wizi.


" Mie nimejifunza kutafuta vilivyo vya halali ili tusipate madhara kama haya," 

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post