SAMIA AMEFANYA MAKUBWA MIAKA 3 TUTAMLIPA 2025

Rais Samia ameendelea kufanya maajabu kwa kuendeleza miradi mikubwa ya maendeleo na kuweza kuibua mipya ambapo anaifanya nchi ya Tanzania kung'ara katika kuitendea haki nchi hii kwa uzalendo na haki.


Hayo ameyasema leo Mwenyekiti wa Umoja wa vijana Wilaya ya Singida Mohamed Jumanne Msaghaa alipokuwa Mbashara Standard Radio asubuhi ya leo katika kipindi cha Zinduka kinachoendeshwa na Amini Nyaungo pamoja na Charles Kikoricho.

Msaghaa ameweka wazi kuwa Rais Samia ameweza kuipata thamani Mkoa wa Singida hususani katika miradi ya maendeleo, Hospital ya Wilaya katika kufanya ukarabati wa Hospital ya ,Shule ya Imbele, kituo cha Afya cha Sokoine kinaendelea kukaratabiwa na huduma zinaendelea kutolewa.

"Tunaamini kwa kipindi Rais amefanya vizuri sana, na tunaimani na Rais Samia kwa kazi nzuri anayoifanya kwa huduma kupelekwa karibu na jamii," Msaghaa.

Ameweka wazi kuwa katika uchaguzi ujao Rais Samia ataendelea kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi.

Katika kipindi cha mwaka mmoja alichokaa Msaghaa madarakani ameweka wazi yale makubwa ambayo ameyafanya ni pamoja na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo aliyoyafanya ikiwemo.


"Tumefanya ziara ya umoja wa vijana wa CCM Wilaya kwenye kata zote 18, tumeanzisha ligi ya mpira wa miguu UVCCM Singida Mjini Cup, tumeibua hamasa ya vijana kuweka pamoja, Tumeendelea kutatua changamoto za vijana kwa kuwapa jezi , mipira na kuwasemea kwenye fursa," Msaghaa.

Katika hatua nyingine Msaghaa aliambatana na  Masatu Bure  Salum Mwenyekiti Seneti UV-CCM vyuo na Vyuo vikuu mkoa wa Singida,  amesema Rais Samia ameweka mipango mizuri ya kupata mikopo katika kipindi cha miaka 3 sasa inapatikana kwa wepesi mno. 

Amesema kuwa vyuo vya kati watu wanapata mikopo akitanabaisha kuwa hii haijawahi kutokea. 


"Katika kipindi cha nyuma hakuna aliyewahi kupata mikopo watu wa vyuo vya kati watu Diploma wanapata mikopo na wanaendelea na masomo," Msatu. 

Masatu amesema kuwa Rais Samia aliyoyafanya wanajambo lao ili kulipa mema aliyoyafanya akiyataja moja wapo ni kuyaelezea yale makubwa lakini pia kumpa kura zote za ndio 2025.

Mwisho.. 

Post a Comment

Previous Post Next Post