ELIMU YA MFUMO WA e-ARDHI YATOLEWA KUPITIA STANDARD RADIO.

 


NA MWANDISHI WETU, SINGIDA



Wataalamu wa ardhi kutoka Mkoa wa Singida, wakiambatana na wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, wametoa elimu kwa wananchi wa mkoa huo kuhusu matumizi ya mfumo wa e-Ardhi, unaowawezesha wananchi kupata huduma mbalimbali za ardhi kwa njia ya kidijiti.



Elimu hiyo imetolewa leo, Septemba 18, 2026, kupitia Standard Radio, ikiwa na lengo la kuwasaidia wananchi kuelewa namna ya kutumia mfumo huo katika kupata huduma za ardhi kwa urahisi na kwa wakati.



Wataalamu hao wameeleza kuwa kupitia mfumo wa e-Ardhi, wananchi wanaweza kufuatilia na kupata baadhi ya huduma za ardhi bila kulazimika kufika mara kwa mara katika ofisi za ardhi. Aidha, wananchi wamehimizwa kujifunza na kutumia mfumo huo kwa usahihi, huku wakitakiwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika endapo watakutana na changamoto katika matumizi ya huduma hizo.



Kwa upande wa Kamishna wa Ardhi Msaidizu Mkoa wa Singida Shamimu Hoza amesema Mkoa umejipanga vyema kuupokea mfumo huo  na wataendelea kutoa elimu kwa jamii ili uwasaidie kuondoa migogoro ya ardhi.



"Singida tupo tayari kwa ajili ya kuusimamia mfumo huu ambao utaondoa kwa kiasi kikubwa migogoro ya ardhi," Amesema

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post