HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » HANJE ATEKELEZA AHADI VIJANA WAMPONGEZA MUNGAA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Nusrat Hanje leo ametoa mipira sita kwa timu za mpira wa miguuu katika kata ya Mungaa na Makiungu ikiwa na lengo la kukuza na kuendeleza vipaji. 
Hayo yamefanyika leo katika Tarafa ya Mungaa, Kata ya Mungaa pamoja na kata ya Makiungu, baada ya Mheshimiwa Hanje kuwaahidi viongozi wa timu hizo walipokutana Puma siku ya jana na kuamua kutekeleza ahadi yake kwa vijana hao leo. 

Hanje amesema kuwa katika kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kupenda michezo lakini pia akisema kuwa michezo ni afya pamoja na biashara nayeye anaendeleza utamaduni huo kwa vijana.

Amesema alipokutana na viongozi wa timu hizo walikuwa na shida ya mipira hivyo akaona ni vyema kutekeleza ahadi hiyo ili waendeeleza vipaji na ndoto zao.

"Nimekutana na kundi kubwa la vijana siku ya jana katika mkutano pale Puma vijana hawa walikuwa na shida ya mipi
ra ambao wanatoka katika kata mbili za Mungaa na Makiungu, leo nineamua kuwapa mipira na bado nitaleta jezi na mambo mengine mazuri kwa ajili yao, " 

Hanje ametumia nafasi hiyo kuwaasa vijana kujitunza na kuendeleza amani iliopo ili Shughuli mbalimbali za maendeleo zifanyike kwa uhuru. 
Amewaomba vijana kutumia muda wao wa ziada kufanya mazoezi hiyo itasaidia kuwaondoa katika makundi mabaya. 

Mwisho amewaalika katika tamasha la kuupokea Mwenge ww Uhuru ambapo mkoani Singida utaingia tarehe 07.07.2024 akisema kuwa kutakuwa na mambo mengi na mazuri kwa vijana. 
Kwa upande wao vijana kwa ujumla wamefurahishwa na utekelezaji wa ahadi ya Mbunge Hanje wakipongeza juhudu za Rais Dokta Samia Suluhu Hassan katika kuleta Maendeleo katika michezo na sekta nyingine. 

Mwisho. 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

2 comments: