HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » TULAANI TUKIO LA MAUAJI YA MTOTO KAGERA- KAJULA


Watanzania wametakiwa kuwa na upendo pamoja na kuhurumiana kama ilivyo desturi ya nchi hii, kitendo hiki itapelekea kutokuwepo na vitendo vya ukatili wa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).

Hayo ameyasema leo Juni 21,2024 Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Singida Ambwene Kajula ofisini kwake akitoa pole kwa familia iliyompoteza mtoto wao Asiimwe Mkoa Kagera kwa kuchukuliwa na watu wasiokuwa wema na kumpotezea maisha na kuchukua  baadhi ya viungo vyake. 

Kajula amelaani tukio hilo la mauaji ya mtoto huyo huku akiwaomba Watanzania kuwa na hofu ya Mungu katika mambo mbalimbali.

Kajula amekemea vitendo hivyo na kutoa maagizo kwa Mashujaa wote  kuwa walinzi katika jamii wanazotoka pia waweze kuangalia namna gani wanawalinda watu wenye Ualbino. 


"Natoa maagizo kwa Mashujaa wote Mkoa Singida, tuzilinde jamii pamoja na kuwaangalia kwa Karibu watu wenye Ualbino kwani nawao wana haki ya kuisjikama tulivy sisi," Kajula

Aidha Kajula ameungana na viongozi wa kitaifa kulaani tukio la kinyama la mauaji ya mtoto Asimwe Novati lililotokea mkoani Kagera. 


 Mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply