MZUNGUKO WA SINGIDA UWEKE MDUDU NYUKI, MGOMBEE UONGOZI VIJANA- MSAGHAA


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Singida Mohamed Msaghaa amesema kuwa atashauri  iongezwe alama ya mdudu nyuki katika zile  alama zilizowekwa katika eneo la mzunguko mkoani Singida ambapo alama hizo zinaonesha alama ya baadhi ya VITU vinavyopatikana mkoani hapa.



Hayo ameyasema leo katika Shamba Darasa liliotolewa na Mohamed Omary Maarufu kama Majengo Nyuki darasa lililohusu umuhimu wa nyuki katika kuchavusha mazao ambayo iliyofanyika Kijiji Cha Manga mkoani Singida ambapo katika hotuba yake Msaghaa amegusia kuwa katika eneo hilo l mzunguko inatakiwa iongezwe alama ya nyuki kwani ni moja ya rasilimali inayopatikana mkoani Singida.


" Nitashauri uongozi wa mkoa wa Singida waongeze picha ya mdudu nyuki katika eneo la Round About ya Singida kwani nyuki ni alama muhimu inayopatikana Singida," Msaghaa.



Aidha katika hotuba yake amewahimiza Vijana kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa Vijana wajitokeze kwa wingi kuomba nafasi za kuongoza ili wawe sehemu ya maamuzi.

"Nawashauri Vijana wenzangu msiache kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kama unaouwezo wa kuongoza nitajisikia faraja kama mtajitokeza kwa wingi kuomba uongozi," Msaghaa.


Katika darasa hilo alikuwepo Afisa nyuki Mwandamizi Halmashauri ya Manispaa ya Singida Gaudence Emil Kazyoba amewaahidi kushirikiana na Majengo Nyuki kukuza kazi yake huku akiwaomba Vijana kujiunga na vikundi mbalimbali ili mikopo itakavyokuwa tayari wapate 



Pia amesema Kuna mfuko wa Misitu wakijunga katika vikundi wanaweza kupata mikopo na ameweza kuviunganisha vikundi mbalimbali ikiwemo Mwankoko,Unyianga na Unyambwa na Sasa wanaendelea vizuri na vikundi vyao.



Katika darasa hilo Majengo ameiomba serikali kuwatengenezea mazingira rahisi ambayo yatawafanya kufanya kazi zao kuwa rahisi.


Mwisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post