Na Amini Nyaungo
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Singida limeanza oparesheni maalum ya kuwasaka na kuwachukulia hatua kali watu wote wanaojihusisha na uharibifu wa miundombinu ya umeme pamoja na wizi wa nishati hiyo.
Ambapo tayati imeiomdolea huduma nyumba moja iliyo maeneo ya Minga Mkoani Singida kwa kuiba umeme ambao umeunganishwa na "Vishoka"
Akizungumza Mdhibiti Mapato wa TANESCO Mkoa wa Singida, Mhandisi Lugano Mwakinyala, amesema oparesheni hiyo inalenga pia kukomesha vitendo vya wananchi kujiunganishia umeme kinyume cha taratibu kwa kutumia mafundi wasio rasmi maarufu kama vishoka.
Amesema kuwa baada ya kuishika nyumba hivyo wanaondoa huduma za umeme kwani mkta iliyofungwa hapo hawaitambui.
"Opararesheni hii inalenga kukomesha wizi na hii nyumba tunaondoa huduma hii kwakuwa hii mita hatuitambui," Lugano
Aidha kwa upande wa udhiniti mapato Augustino Shirima amesema kuaa waliounganisha umeme katika nyumba hiyo wametumia mbinu ambazo umeme unaingia moja kwa moja hausomi katika mita ambayo imefungwa.
Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kutumia huduma rasmi ya Nikonekt ya TANESCO ili kupata maombi ya umeme kwa njia salama, rahisi na ya haraka, badala ya kutumia njia zisizo halali ambazo huweka maisha na mali zao hatarini.
Shirika hilo limeahidi kuendelea na oparesheni hiyo katika wilaya zote za Mkoa wa Mwanza hadi vitendo vya hujuma na wizi wa umeme vita kapokoma kabisa.
Mwisho.


Post a Comment