Na Amini Nyaungo
Timu ya soka ya Singida Black Stars imekuja na kampeni ya karata tatu kuelekea michezo yao mitatu ya ligi Kuu soka Tanzania Bara na kombe la Shirikisho la Soka Tanzania ikiwa na lengo la timu hiyo kushinda michezo hiyo.
Hayo ameyasema leo Afisa Habari wa timu ya Singida Black Stars Hussein Masanza alipoongea na Waandishi wa Habari Mkoani namna ya kuitekeleza kampeni hiyo ambayo itachezewa katika uwanja wao mpya wa Airtel uliopo eneo la Mtipa mkoani hapa.
Masanza amesisitiza kuwa ni muhimu sana kwa kila mmoja kufika kuangalia mpira kwa kwa sasa wameamua kurudi katika sehemu zao katika msimamo.
Lakini pia amegusia umuhimu wa.michezo yote ikiwemo mchezo wao dhidi ya Yanga utakao chezwa 05,03,2026, Coasta Union utachezwa 02,03,2026 hizi zikiwa za ligi kuu Tanzania Bara pamoja na Songea United katika kombe la Shirikisho ambao utachezwa tarehe 07.03.2026.
Aidha ametumia nafasi hiyo kuwaomba mashabiki kufika uwanjani ili waangalie burudani nzuri ya soka.
"Mashabiki mfike muone mpira itakavyopigwa katika uwanja wetu kwani tumejiandaa vizuri kuelekea katika karata tatu,"Masanza.
Mwisho



Post a Comment