Na Mwandishi Wetu,Mkalama
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Hajjat Asia J. Messos, leo Julai 8, 2026 amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Kata za Kinampundu, Mwanga na Nkalankala.
Katika ziara hiyo, Hajjat Asia Messos ametembelea na kukagua miradi yenye thamani ya jumla ya Shilingi 480,195,000 inayolenga kuboresha huduma za elimu na afya kwa wananchi wa Wilaya ya Mkalama.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na:
Ujenzi wa Vyumba 6 vya Madarasa, Jengo la Utawala, Matundu 16 ya Vyoo na Madarasa Mawili ya Mfano katika Shule ya Msingi Grace Mesaki.
Ukamilishaji wa Vyumba Viwili vya Maabara katika Shule ya Sekondari Seth Benjamini.
Ukamilishaji wa Chumba Kimoja cha Maabara katika Shule ya Sekondari Selenge.
Ukamilishaji wa Chumba Kimoja cha Maabara katika Shule ya Sekondari Grace Mesaki.
Ukamilishaji wa Zahanati ya Malaja.
Ujenzi wa Matundu 24 ya Vyoo katika Shule ya Msingi Nkalankala.
Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji alisisitiza usimamizi madhubuti wa miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati, izingatie viwango vya ubora na iweze kuanza kutoa huduma bora kwa wananchi wa Wilaya ya Mkalama.



Post a Comment