TANESCO SINGIDA WATOA VIFAA VYA KUHIFADHI TAKA MISUNA STENDI KUU

 

Na Amini Nyaungo



Shirika la Umeme Tanzania Mkoa wa Singida (TANESCO) wametoa vifaa vya kuhifadhia uchafu(Dustibin) Stendi Kuu ya Misuna kwa ajili ya kuweka mazingira safi na salama.


Hayo yamefanyika leo Oktoba ,07,2025  ambapo Vifaa hivyo vimetolewa katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambapo wamemkabidhi  mchumi wa Manispaa ya Singida Christopher Ngonyani ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Joanfaith Kataraia.


Ngonyani amesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuuuweka mji wa Singida kuwa katika usafi kwani watakuwa wanahifadhi takataka zao katika vifaa hivyo.


"Vifaa hivi vitasaidia kuiweka Manispaa yetu kuwa salama katika hali ya usafi," Ngonyani


Aidha ametumia nafasi hiyo kuwashukuru TANESCO Mkoa wa Singida kwa kujali na kuwapatia vifaa hvyo.


Kwa upande wa Mhandisi wa Afya na Usalama wa TANESCO Mkoa wa Singida Eng. Nyerere Ernest amesema kuwa wameamua kuwapa vifaa hivyo Stendi ya Misuna kwakuwa ni sehemu yenye watu wengi hivyo itawasaidia kuhifadhi mazingira.


 "Tumeamua kuja hapa kwamuwa kuna watu wengi na itawasaidia kuhifadhi mazingira," Eng. Nyerere



Afisa Uhusiano wa TANESCO Mkoa wa Singida Rehema Mwaipopo pamoja amesema kuwa licha ya kuwaletea vifaa hivyo wataendelea na wiki ya huduma kw awateja pamoja na kutoa elimu mbalimbali za Shirika la Umeme Tanzaniav(TANESCO) linavyofanyakazi pamoja na kuwapa elimu ha gesi safi ya kupikia.




Naye Mwenyekitivwa Wajasiliamali Ismail Kesi amewashukuru TANESCO Mkoa wa Singida kwa kukwa kuwajali kwa kuwaletea vifaa hivyo ambapo wamesema watavitumia kwa uangalifu ili vitumike kwa muda mrefu.


Mwisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post