WAKULIMA WA TUMBAKU MANYONI WAZALISHA TUMBAKU YA DOLA 1,809,382.20


Na Jumbe Ismaily



WAKULIMA wa tumbaku katika vyama vitano vya ushirika vya msingi vilivyopo kata ya Mitundu,Halmashauri ya Itigi,wilayani Manyoni katika msimu uliopita wa kilimo walizalisha jumla ya kilo 736,988 zenye thamani ya dola za kimarekani 1,809,382.20.

Akitoa taarifa fupi ya ununuzi wa tumbaku wakati wa hafla fupi ya kukabidhi madawati 55 kwa ajili ya shule za msingi na milango minne ya kituo cha polisi Mitundu,Meneja uhusiano na Usimamizi wa Kampuni ya tumbaku,Yusufu Mahundi aliweka bayana kwamba kwa mwaka mmoja wamenunua zao hilo na hivi sasa wanaingia mwaka wa pili kununua tumbaku katika wilaya ya Manyoni,hususani katika eneo la Mitundu.



katika Halmashauri nane za mikoa mitano inazofanyaka kazi hapa Nchini ambapo huchangia madawati,visima vya maji,vifaa vya Hospitali,vifaa vya ujenzi pamoja na vifaa vya michezo vyenye jumla ya shilingi milioni 162,832,737.

Alisisitiza kwamba uchangiaji huo unaendana na uzalishaji wa tumbaku wa Halmashauri au kata husika pamoja na mahitaji ya kipaumbele cha wakati huo.

Akikabidhi msaada wa madawati na mageti ya milango,Mkuu wa wilaya ya Manyoni,Dkt.Vincenti Mashinji alipiga marufuku uvamizi wa maeneo ya serikali kwa kuanzisha makazi holela, hata kama lilikuwa ni eneo la umma,shamba la Kijiji,shamba la bega kwa bega,msitu wa Kijiji hairuhusiwi kwenda kufanya shughuli zozote kule bila idhini ya mkutano mkuu wa Kijiji.

MWISHO.


Post a Comment

Previous Post Next Post