MADEREVA WAMETAKIWA KUEPUKA KERO ZA BARABARANI

 

 Na Sylvester Richard.



Madereva wa vyombo vya usafiri mkoani Singida wametakiwa kuacha kero za barabarani zinazoigusa jamii moja kwa moja kwa kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani.



Rai hiyo ilitolewa Februari 26, 2026 na Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Singida, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Elias Mkumbulo, alipokuwa akitoa elimu kupitia Standard Radio Singida.



 Alitaja baadhi ya kero hizo kuwa ni kuendesha bila bima, pikipiki zenye kelele na kuegesha maeneo yasiyoruhusiwa.



Aidha, aliwataka madereva kuzitii sheria ili kuepusha ajali na kuwaomba abiria kutoa taarifa za wanaokiuka sheria kwa makusudi.

Post a Comment

Previous Post Next Post