HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

VIJANA WAILINDE AMANI YA TANZANIA -ZANURA

Na Amini Nyaungo

Vijana wametakiwa kuwa wamoja na kulinda amani ya nchi ya Tanzania kwa kuungana kwa pamoja ili waimarishe undugu pamoja na vuguvugu la kujitolea ii kuleta mapinduzi ya kifikra kwa jamii pamoja na kuhimizana fursa mbalimbali katika jamii.
Hayo ameyasema leo Katibu  wa Taifa letu  Kesho yetu Movement maarufu kama (TK Movement) Zanura Adam walipokuwa wanazindua kampeni hiyo kata ya Merya Mkoa wa Singida ambapo mgeni rasmi alikuwa Diwani wa kata hiyo Iddi Rajabu akimuwakilisha Mwenyekiti wa CCM Halmashauri ya Mnaipsaa ya Singida Vijijini Elia Digha.
Zanura amesema lengo la TK Movement  kuendelea kuwaunganisha vijana na hawafungamani na mtu au chama chochote dini au kabila hivyo yoyote anakaribshwa.

“TK Movement ipo kwa ajili ya kuleta mapinduzi ya kifikra katika jamii, haifungamani na mtu yoyote, dini, chama au kabila,”Zanura

Zanura amewaomba vijana kuungana na TK Movement ili waweze kuwa pamoja , amesema kitaifa ilizinduliwa tarehe 25.05.2024 huku kwa mkoa wa Singida ilizinduliwa tarehe 20.07.2024 kwa  upand wa wilaya ya Singida vijijini imezinduliwa 31.08.2024 leo hii wamezindua katika kata ya Merya.

Kwa upande wake mgeni rasmi wa tukio hilo Diwani wa kata ya Merya Iddi Rajabu amewaomba vijana kubadili na kumrudia Mungu ili kuweza kuondoa mambo ya ajabu yanayoendelea hapa nchini.

Rajabu amesema ni lazima vijana wawe tayari kubadilika na kuwa na hofu ya Mungu ili kila kitu kiwe katika mstari uliokuwa mzuri.
“Vijana wanatakiwa wabadilike wawe katika mstari mzuri wakifanya hivyo kia kitu kitakuwa sawa , wazazi wapeekeni watoto katika mafunzo ya kiimani ili wawe watoto wema,” Iddi.

 Mwisho

MADEREVA WATANO WA MABASI WAFUNGIWA LESINI ZA UDEREVA SINGIDA.

Na Sylvester Richard

Madereva watano wa mabasi ya makampuni tofauti wamefungiwa leseni zao za udereva kwa kipindi cha miezi 3 baada ya  kukamatwa na makosa ya kuendesha mabasi yao mwendokasi usioruhusiwa kisheria ambao ni  zaidi ya Km. 100 kwa saa badala ya Km. 80 kwa saa.

Hayo yamebainishwa na Kamaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)  Mayunga Raphael Mayunga Septemba 19, 2024 alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika Kituo  kukuu cha Polisi Singida.

Aidha, Mayunga amewataja madereva hao kuwa ni Emmanuel Gusha ambaye ni dereva wa Kampuni ya mabasi ya KATARAMA, Habiee Neema Sule wa Kampuni ya mabasi ya MWANAKWETU, Emmanuel Wilson Madaha wa Kampuni ya mabasi ya KATARAMA, Emmanuel Laizer Malambala wa Kampuni ya mabasi ya HAPPY NATION, na Jofu Mnison Kanyika wa Kampuni ya mabasi ya FRESTER.

Mayunga amesema, madereva hao wamekamatwa wakati Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida likiwa katika oparesheni za kubaini, kuzuia na kutanzu uhalifu ambazo hufanyika mara kwa mara ambapo kwa kipindi cha miezi miwili ya Julai na Agosti 2024 oparesheni hizo zilifanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa 137 wa makosa mbalimbali ya jinai ikiwemo watuhumiwa wa mauji, kukutwa dawa za kulevya aina ya bhangi, nyara za Serikali na wizi wa vitu mbalimbali.


WANANCHI WAJITOKEZE KUPIMA AFYA-NYAMIZI

Charles Kikiricho

Wananchi wameombwa kujitokeza  katika vituo vya afya kwaajili ya kupima ugonjwa wa kifua kikuu ili waweze kupata tiba kwani ugonjwa huo unatibika.

Wito huo umetolewa na Daktari wa kifua kikuu Isabela Nyamizi wakati akiongea na Standard Radio asubuhi ya leo 18/09/2024 ya kuwaomba wananchi wajitokeze ili wapime kifua kikuu na watakaobainika waweze kupata tiba. 

Dkt Isabela ametaja miongoni wa dalili za kifua kikuu ni pamoja na kupata homa za usiku, kukohoa damu ,joto kali la mwili nyakati za usiku, kukosa hamu ya kula kwa watoto .

 

Pia Dkt Isabela ametaja makundi ambayo yapo kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi ya kifua kikuu ni pamoja na watu wenye maambukizi ya magonjwa mengine kama vile Ukimwi, Kisukari, watu ambao wanafanya shughuli za uchimbaji madini.

WAKANDARASI WASUMBUFU HAWAFAI KUPEWA TENDA, SAMIA MITANO TENA-IGHONDO


Na Amini Nyaungo
Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Ramadhan Ighondo ametoa rai kwa Wakandarasi wababaishaji wajiangalie na fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Ameyasema hayo jana katika mkutano na wananchi wa Kata ya Ngimu Wilaya ya Singida Vijijini wakati wa kupokea ripoti ya fedha za mradi  ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo, amesema ya kuwa tayari shilingi milioni 687 zimekwisha ingia kwenye akaunti kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Ngimu. 
Ametahadharisha wakandarasi wababaishaji wasipewe tenda wala nafasi katika ujenzi wa kituo hicho maana watakwamisha ujenzi kwa kuwaibia wananchi na kurudisha nyuma juhudi zake za Kuwaletea wananchi maendeleo.

Katika mkutano huo Ighondo ametumia nafasi hiyo kumshukuru  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassani kwa kuwapatia Kwa fedha nyingi za mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya kata ya Ngimu.

"Namshukuru sana Rais Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha Shilingi Milioni 687 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya ambapo ni muda mrefu tangu wananchi wajitolee nguvu kazi ambapo wakajenga boma lakini halikufanikiwa kukamilika," Amesema
 
"Ni miaka 14 ndugu zangu lakini tangu niingie madarakani nimepambana vya kutosha kila nilipopata fursa nilikisemea kituo hiki sasa kitajengwa kuanzia msingi mpaka kikamilike". Rais Samia ametupatia fedha nyingi jimboni kwenye miradi mingi sana na sisi hatuna deni naye tunamwahidi kumpa mitano tena aendelee kuwaletea wananchi Maendele," Ighondo

Pia amewaomba wananchi kutoa taarifa kwa yeyote yule atakayehujumu fedha za Mradi huo ili kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Pamoja na hayo ametoa wito kwa jamii kusimama imara kulinda na kutunza Miundombinu yote katika miradi iliyojengwa katika Kata hiyo ikiwemo maji,umeme, Barabara, zahanati na vyumba vya Madarasa shuleni.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Dr. Grace C. Ntogwisangu amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho utaanza mapema Mwezi ujao huku akitilia mkazo kwa Wananchi kuchangia nguvu kazi ya  20% ili ujenzi huo ukamilike. Amewataka wasimamie fedha hizo ili ujenzi ukamilike kwa wakati.
Wananchi wa kata ya Ngimu wamemshukuru Ighondo kwa kuwatetea bungeni wamemuomba aendelee na kujituma wao ndio wataamua wakati ukifika.


Mwisho

WANAWAKE WAPATE KIPAUMBELE KUKOPESHWA BENKI

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanawake nchini kutumia fursa ya mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa ajili ya kukopa na kujiongezea vipato.

Dkt. Biteko ametoa rai hiyo mkoani Singida wakati akimwalilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kwenye Kilele cha Maonesho ya Saba ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji kwa Mwaka 2024.


Dkt. Biteko amebainisha kuwa Rais Dkt. Samia alitoa wito kwa benki kuongeza kiwango cha kutoa mikopo kwa wananchi huku akitolea mfano Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ambayo mwaka 2020 ilitoa shilingi bilioni 63 na hadi kufikia Agosti 2024 imetoa mikopo kiasi cha shilingi bilioni 337.
Ametaja takwimu za utoaji mikopo hiyo kutoka Benki ya TADB kuwa wanaume ni asilimia 58.1, vijana asilimia 19 na wanawake asilimia 22.4 huku akisisitiza benki nchini kuendelea kuongeza kiwango cha utoaji mikopo kwa wanawake.

Sambamba na hayo Dkt. Biteko amezindua Mwongozo wa Uratibu na Usimamizi wa Mifuko na Programu za Uwezeshaji ili iwe nyenzo ya kuimarisha utendaji wa mifuko na programu za uwezeshaji kwa lengo la kuondoa changamoto zilizopo hasa mikopo chechefu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini katika jamii.

Mwisho

AKITOKEA KIONGOZI ASIYE NA FEDHA ANA SERA NZURI MCHAGUENI-BITEKO


Na Amini Nyaungo
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dokta Dotto Biteko amewaomba wananchi wa Singida kuchagua viongozi walio na sifa ambao wataweza kuweka msingi imara wa uongozi na kuwaletea maendeleo.

Biteko ameyasema hayo leo katika Maonyesho ya Saba ya Uwezeshaji yaliyofanyika mkoani Singida ambapo yeye amemuwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

"Chagueni viongozi walio na sera nzuri zitakazoweza kutatua shida zenu, msichague viongozi kwa urafiki na wasiokuwa na sifa'" Biteko
Ametoa wito kwa Benki zote kuwaamini wanawake katika utoaji wa mikopo ili iwasaidie katika shughuli zao anaamini wanawake wanaweza kuzilinda familia.

" Nitoe wito kwa Benki zote wawape kipaumbele wanawawake katika kuwakopesha fedha ili walete maendeleo," amesema

Pia amezindua Muongozo wa Mifuko na Program za Uwezeshaji wananchi pamoja na kutoa vyeti kwa makundi mbalimbali.

 Biteko hakuacha kumpongeza mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego kwa kazi nzuri aliyoifanya kuandaa maonyesho  haya.
Amewaomba wananchi wa Singida kupendana akieleza kuwa endapo wanapenda uchumi utakua na maendeleo yatakuwepo.

Mwisho

WASHIRIKI MAONYESHO YA UWEZESHAJI SINGIDA WAFURAHI WADAU WAFIKA

 

Na Amini Nyaungo

Maonyesho ya saba ya Uwezeshaji yanaendelea mkoani Singida ikiwa kesho Jumamosi ndio tamati ya maonyesho hayo Naibu Waziri Mkuu Dokta Dotto Bitteko atakuwa mgeni rasmi, wadau na washiriki wafurahishwa na maonyesho hayo.

Chamber Media imetembelea washiriki ambao ni Taasisi na Kampuni mbalimbali kwa ujumla wake wafurahishwa na maonyesho huku walio wengi wamepata kile walichofuata.


Aurelia Masasi yeye ni Afisa Uwekezaji wa EFTA amesema wamekuja mkoani Singida kuonesha bidhaa walizokuja nazo ikiwemo "Power Tila" naTrekta ambazo wanakopesha na kupitia maonyesho hayo watu wawili wameshanunua bidhaa yao.

"Tumefurahishaa na hizi tunaendelea kuwaita wadau na watu mbalimbali kutembelea banda letu ili wajionee na wakipendezwa wachukue bidhaa zetu," Aurelia.

Naye Amina Hassani Mkurugeni wa Kampuni ya bidhaa za nyuki "Mwangaza Honey Food Company" ametokea mkoani Tabora.

Yeye amewakaribisha wadau lakini pia amewataka wafike bandani kwao ili wapate kuona bidhaa nzuri kutoka kwao.
Naye Victoria Emanuel wanajihusisha na madawa ya mifugo ambapo wametumia fursa hiyo kuitangaza biashara kwa kuwa ndio wanaanza.

Manji Jackson kutoka NHIF wao wapo hapo akisema mahudhurio mazuri sana banadani kwao na wanaendelea kuhimiza watu kujiunga na mifuko ya hifadhi ya Jamii.

Mwisho