UISLAM MKOA WA SINGIDA UMEANZIA KITITIMO

 Na Mwandishi Wetu



 Eneo hili Tulizuru Jana 15 juni 2025 na Baadhi ya makhalifa na wakiwepo wenyeji wa Eneo Hilo ndio Uislamu ulianzia Hapa na Bi Mayasa Binti Ufunguo na Baadae kumkaribisha Sheikh khalid Sudi,


 Ambae aliwafundisha wanazuoni wakubwa kama vile akina Sheikh Hassan Mpondo wa Mitunduruni na Sepuka akipelekwa Sheikh Swalehe Chambia kueneza Dini ya Kiislam.


 Ndugu zangu eneo hili ndio hali ya Msikiti ulivyo huo ni Nembo ya Uislamu Mkoa imeanzia hapa natumai tutashikaman ili kuuweka Msikiti huu katika Hadhi nzuri.


 Ni aibu pia kutouweka katika Mazingira Mazuri kila Muislamu aliepata Athari ya huyu Bibi kupitia hawa masheikh tuupambanie huu Msikiti inshaallah 


NI mimi khalifa wa Makhalifa wote Kata ya Sepuka Mji wa Kistaarabu

Post a Comment

Previous Post Next Post