Na Jumbe Ismailly SINGIDA
HALMASHAURI ya Manispaa
ya Singida imetoa mikopo kwa vikundi 16 vya wanawake pamoja na vijana katika
kata ya Kindai yenye thamani ya shilingi milioni 68,500,000/= ili kuviwezesha
vikundi hivyo kukuza uchumi na kujiongezea kipato katika kipindi cha kuanzia
mwaka 2020 hadi mwaka 2025.
Diwani wa Kata ya
Kindai,katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida,Omari Salumu maarufu kwa jina
la Kinyeto aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika mtaa wa
Kibaoni alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM).
Aidha diwani Kinyeto hata
hivyo alifafanua kwamba kati ya kiasi hicho cha fedha,shilingi milioni
55,500,000/= zilitolewa mikopo kwa vikundi 16 vya wanawake na vijana kwa
kipindi cha mwaka 2020 hadi juni,mwaka 2024 na shilingi milioni 13 zilitolewa
mikopo kwa vikundi vitatu vya wanawake kuanzia mwezi julai,mwaka jana hadi
mwezi Aprili mwaka huu.
“Hizo ndio fedha taslimu
ambazo zimeletwa katika Kata ya Kindai na vikundi hivyo vyote vimepewa na
vingine vyote vimeweza kurejesha na bado kuna vikundi vichache havikuweza
kurejesha,lakini pia baada ya serikali kufanya mabadiliko ya muundo mzima wa
utoaji wa fedha za mikopo vikundi vitatu vimeweza kukidhi vigezo na vimeweza
kupewa fedha na jumla ya fedha iliyoweza kutolewa ni shilingi milioni
13”alifafanua diwani huyo.
Hata hivyo Kinyeto
aliweka bayana kuwa kutokana na mabadiliko ya utoaji wa mikopo hiyo kufanyika
hivyo aliwataka wanawake vijana na watu wenye ulemavu kwenda kwa maafisa
watendaji wa kata kwa ajili ya kupatiwa maelekezo ya taratibu ambazo zinaweza
kukidhi vigezo vya kupatiwa mikopo hiyo ili na wao waweze kupatiwa.
Alisema diwani huyo
kupitia Chama Cha Mapinduzi kwamba katika kipindi cha mwaka mzima Kata ya
Kindai ilikusanya jumla ya shilingi milioni 17 lakini pamoja na kiasi hicho
kidogo walichokusanya,serikali kuu iliipatia kata hiyo shilingi bilioni 3.1 kwa
ajili ya kukamilisha miradi mbali mbali ya maendeleo.
Hata hivyo diwani huyo
kijana alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania,Daktari Samia Suluhu Hassani kwa kuipatia kata hiyo jumla ya shilingi
bilioni 3.1 zilizowawezesha kufanikisha miradi ya ujenzi wa shule,miundombinu
ya barabara,ofisi za serikali za mitaa pamoja na kuviwezesha vikundi vya
wajasiriamali mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana.
Naye diwani wa viti
maalumu tarafa ya Mungumaji,Rehema Ntandu aliwasihi wale wote walioboresha
taarifa zao kwenye daftari la kudumu la mpiga kura na wenye sifa za kupiga kura
wajiandae kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu
MWISHO.
Post a Comment