Na Jumbe Ismailly SINGIDA
DIWANI wa Kata ya Kindai.katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida,Omari Salumu maarufu Kinyeto amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya uwakilishi wake kata ya Kindai imepokea jumla ya shilingi bilioni 2,468,740/=kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara ya juu kwenye ziwa kindai na munangi pamoja na ujenzi wa kivuko cha chini ili kukabiliana na ajali za barabarani katika Kata hiyo.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mkutano wa hadhara aliofanya katika mtaa wa Kindai,diwani Kinyeto alisema kwamba kati ya kiasi hicho cha fedha zaidi ya shilingi bilioni 1.9 zilijenga miundombinu ya barabara ya juu kwenye ziwa Kindai na Munangi na shilingi 568,740,000/= zilijenga kivuko cha chini.
“Ujenzi wa kivuko cha chini utaona pale katika shule ya msingi Mahembe na Kibaoni tulikuwa tunapokea matukio mengi sana ya ajali wanafunzi walikuwa wakienda shule wakivuka wanakutana na adha wengine wanagongwa na magari kulikuwepo na vurugu kubwa sana katika eneo hili….
Kiasi cha kwamba siku moja magari yanayotoka Mwanza kwenda Benki kuu gari moja ilimgonga mtoto na kufariki na wananchi walichukua sheria mkononi wakafunga barabara ile wakachoma na matairi ikatokea tafrani kubwa sana”alifafanua Kinyeto.
Kwa mujibu wa diwani huyo lakini baada ya seriakli kusikia kilio hicho ikaamua kuwapatia shilingi milioni 568,740,000/=kwa ajili ya kukamilisha kazi ya ujenzi wa kivuko cha chini ambapo kwa hivi sasa wanafunzi wanapita chini na hawavuki tena kwa juu na kusisitiza kuwa tangu kivuko hicho kilipokamilika hapajawahi kutokea tukio lolote la mwanafunzi kugongwa wala mwananchi yeyote kupata ajali.
“Nitakuwa mnyimi wa fadhila iwapo sitaweza kumshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Daktari Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa anayofanya ya kuhakikisha anawagusa wananchi wake na hana ubaguzi katika ugawaji wa fedha za maendeleo katika nchi yetu ya Tanzania” alifafanua mwakilishi huyo wa wananchi wa Kata ya Kindai.
Kwa upande wake diwani wa viti maalumu Manispaa ya Singida,Rehema Mande aliwahamasisha wananchi wa kata ya Kindai kutunza vichinjio vyao ili utakapofika mwezi wa kumi waweze kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura za kumwagika kwa nafasi ya Rais,Daktari Samia Suluhu Hassani.
“Sisi akina mama huwa tuna mambo mengi lakini mie nawasihi akina mama wenzangu tuvitunze vizuri na akina baba pia na vijana wetu ili mwezi wa kumi tukatoe kura za kumwagika siyo za kishisndo kwa mama Samia kutokana na mambo mengi ambayo ameyafanya na yanaonekana katika mikoa yote,wilaya zote,kata zote na vijiji vyote mama Samia kafanya kazi nzuri sana”alisisitiza
Akichangia taarifa hiyo ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa CCM,Edward Anthoni Mlacha alisema katika kipindi cha miaka isiyopungua 20 tangu alipohamia Kindai hawajaweza kupata barabara ya lami kwa miaka ya nyuma,lakini katika kipindi cha miaka mitano ya uwakilishi wa diwani anayemaliza muda wake mtaa wa Kindai wamepata barabara ya lami.
MWISHO.
Mwisho
Post a Comment