SMAUJATA SINGIDA WATOA POLE KWA MAFURIKO NA AJALI YA GARI


Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Singida Ambwene Kajula amewapa pole wananchi mbalimbali waliopatwa na majanga ya mafuriko pamoja na ajali ya gari kwa wanafunzi mkoani Arusha. 


Ambwene amesema hayo leo ya kuwa amesikitishwa na mafuriko yaliyotokea Rufiji Mkoani Pwani pamoja na Mkoani Mbeya baada ya kumeguka kwa mlima ambao umesababisha nyumba ishirini kubomoka. 

Aidha Kajula maetumia fursa hiyo kuwaomba wasamalia wema kusadia watu waliopatwa na dhoruba hiyo ili kila mmoja awe katika wakati mzuri wa kuishi.

"Nasikitika kutokea kwa mafuriko mkoani Mbeya na Rufiji kwa pamoja sisi kama SMAUJATA mkoa wa Singida tupo pamoja nao nawaomba wasamalia wema kutoa misaada ili kuzifarji kaya zilizokosa makazi nao wafurahie maisha kama zamani, "Kajula 

Katika hatua nyingine Kajula ametoa pole kwa ajali ya gari kwa wanafunzi mkoani Arusha huku akiwaomba madereva kuwa makini kutoendesha kwa kasi ili kuokoa maisha ya watoto. 

"Niwambe madereva kuwa makini wanapoendesha magari kwani kuna ajali nyingine zinaweza kuzuilika endapo mwendo ukiwa wa kawaida," Kajula. 

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post