RC SINGIDA ATAKA UWAJIBIKAJI KWA WATUMISHI WALIOKUSANYA PESA


Na Mwandishi Wetu



Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, ametoa siku saba kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida kuwasilisha fedha zaidi ya Sh.milioni 6 walizokusanya katika vyanzo mbalimbali vya mapato lakini hawakuziwasilisha benki kama taratibu na sheria zinazoelekeza.



Akizungumza katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

Kikao hicho kilikuwa cha kujadili hoja zilizoibuliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),

Mkuu wa Mkoa Halima Dendego, amesema haiwezekani hoja ya Sh.milioni 6 iendelee kuwepo wakati wahusika wanaotakiwa kulipa fedha hizo wapo.

Aidha ameiagiza ofisa ya Utumishi katika halimashauri hiyo kuwachukulia hatua  watumishi wanaodaiwa fedha hizo kwa wahawezi kuona hoja ya Sh.milioni 6 iliendelea kuichafua halmashauri.

Katika hatua hiyo ameagiza ndani ya siku saba watumishi waliohusika watafute popote na kulipa pesa hizo ndani ya siku hizo saba.

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post