Dereva wa Bajaji mkoani Singida aliyefahamika kwa jina moja la Abdallah anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa baada ya kuhusishwa na hatia ya kumtia mimba mtoto wa shule ya Sekondari Mughanga anayesona kidato cha pili mwenye miaka 14 jina lake limehifadhiwa.
Akizungunzia taarifa hiyo Mwenyekiti wa SMAUJATA Manispaa ya Singida Miraji Hamis amesema kuwa walipata taarifa ya tukio hilo leo baada mwaanchi mwenye nia njema kupenyeza ujumbe huo na kuanza kufuatilia na hatimaye wamempata mtuhumiwa eneo la Mnung'una alipokuwa anakimbia.
Baada ya kufuata utaratbu wote SMAUJATA kwa kushirikiana na jeshi la Polisi wamemkamata mtuhumiwa na sasa yupo mahabusu kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
PICHA YA MWENYEKITI SMAUJATA MANISPAA YA SINGIDA MIRAJI HAMIS
Miraji ametumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuacha tamaa ya kushiriki mapenzi na watoto wadogo hasa wanaosoma shule kufanya hivyo kunawaharibia ndoto za maisha yao ikiwemo kuwa viongozi wakubwa wa nchi.
Bibi wa mtoto huyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake ameiomba serikali na jeshi la polisi kuwadhibiti watu kama hao wanaoharibu watoto wao wakiwa wadogo.
Amesema kuwa alimgundua mjukuu wake kuwa ana mimba baada ya kumuona amebadalika mwili na mambo mengine yanayoashiria mimba.
" Serikai isiwaache watu kama hawa , wanaharibu taswira nzima ya watoto wetu, sheria ifuate mkondo wake, " amesema.
Mtoto mwenyewe (Jina limehifadhiwa) amesema kuwa Abdallah alimwambia anampenda sana, alipo ulizwa ya kuwa nini alipewa mtoto huyo akajibu hakuwahi kumpa kitu chochote bali maneno ya kumpenda ndio alikuwa anamwambia.
Wapi walikuwa wanakutana amesema kuwa Jamatini kattkati ya mkoa wa Singida ambapo Abdallah alikuwa anapaki.
Makamu Mwenyekiti wa SMAUJATA mkoa wa Singida Elineema Babu aliambatana na Miraji Hamis katika tukio hilo naye amewahimiza wazazi kuwa waanawalifu na kuwajengea ukaribu pamoja na urafiki ili waweze kueleza yae yanayowakabili.
Babu ameomba vijana wanapofika umri wa kuoa waoe ili waepuke na tamaa kwa watoto wadogo wenye ndoto kubwa za kuwasaidia wazazi wao.
"Nachukizwa sana na mtukio haya, mimi ni mzazi nina watoto pia tukio kama hili naona kama tukio langu ndio maana tu pambana usiku kucha kuondoa matukio kama haya, "Babu
*KATAA UKATILI WEWE NI SHUJA.*

Post a Comment