MAMA NTILIE WAPIKIA NISHATI SAFI ,TANESCO SINGIDA WATOA ELIMU

 Na Amini Nyaungo



Wajasiliamali  waipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO ) Mkoa wa Singida kwa kuwapa elimu Mbashara ya matumizi ya Gesi safi ya kupikia inayotumia nishati ya umeme pamoja na kulika chakula wakiwa katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi Msufini Manispaa ya Singida.



Wameyasema leo Oktoba 08,2025 walipokuwa wanapewa elimu kutoka kwa maafisa wa TANESCO wa Mkoa wa Singida wakati huu wa wiki ya huduma kwa wateja.


Mama lishe Asha Ramadhani amesema kuwa kupitia elimu waliyoipata kutoka TANESCO wataendelea kuitumia na kuahidi kuwa elimu hiyo wataisambaza kwa wengine ili watumie nishati hiyo.



"Tumeipata elimu hii leo na mimi nitaendelea kuitoa kwa wengine ili watumie nishati safi, nawashukuru TANESCO kwa kutupa elimu hii," Amesema.


Aidha Halima Juma amesema kuwa amepika kwa kutumia nishati safi ya Umeme kwa kutumia muda mchache kuivisha chakula hivyo akisema kuwa  ni nzuri na ataishawishi familia yake ili wanunue gesi safi ya kupikia ya Umeme.


"Nimetumia muda mchache sana leo nimepika wali, nyama na pilau kwa muda mchache sana hii ni nzuri mno,'' Aisha


Kwa upande wake Afisa Uhisano wa Shirika la Umeme Mkoa wa Singida Rehema Mwaipopo amesema kuwa siku ya leo wamtoa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ambayo ipo vizuri ba wameikubali.


Aidha Mwaipopo amesema kuwa licha ya kuwapa elimu bado wamepika  Mbashara na mama lishe pamoja na wananchi waliojitokeza hapo ili kuwaonesha namna inavyofanya vizuri.


"Leo tumewapa elimu ndugu zetu juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia lakini pia tumepika nao pamoja leo," Mwaipopo.


Mwisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post