Na Mwandishi Wetu
Hand in Hand Eastern Africa Tanzania imefanya jukwaa la mahusiano ya kibiashara kwa wadau katika soko la kuku (Market linkage) ikiwa na lengo la kujenga soko lenye fursa na mahusiano madhubuti ya kibiashara kati wanufaika wa miradi ya Hand in Hand wanaojihusha na ufugaji wa kuku na wanunuzi mbalimbali.
Akiongea leo Lucas Augustino Michael ambaye ni Meneja wa Miradi Mnyororo wa thamani amesema kuwa kuwepo kwa jukwaa hilo wanaamini kwamba wamewaunganisha wazalishaji na wanunuzi, pamoja na kuimarisha upatikanaji wa masoko yenye tija, kuongeza mauzo, na kuwawezesha wanufaika wao kukuza biashara zao kwa ufanisi zaidi.
Jukwaa hili limetoa nafasi kwa wadau mbalimbali kukutana, kujadiliana, kubadilishana uzoefu na maarifa muhimu, pamoja na kuchunguza fursa za ushirikiano zitakazonufaisha biashara binafsi na sekta ya ufugaji wa kuku kwa ujumla.
Aidha, kulikuwa na mijadala ya kitaalamu, mada za viongozi wa sekta, pamoja na vipindi vya mawasiliano na ushirikiano vitakavyowezesha washiriki kujenga mahusiano yenye tija na kuchangia maendeleo ya sekta ya ufugaji wa kuku.
Katika jukwaa hili Hand in hand wamewaalika wadau wote katika mnyororo wa thamani wa sekta ya ufugaji wa kuku kushiriki katika tukio hili.
Mwisho.


Post a Comment