KISHOA AIBANA SERIKALI KUELEZA MKATABA WA KAMPUNI YA SONGAS

Na Emanuel Dangote



Mbunge wa Iramba Mashariki, Jesca David Kishoa, ameitaka Serikali kueleza hatma ya mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya SONGAS, akitaka kufahamu iwapo mkataba huo uliongezwa au ulivunjwa baada ya kumalizika muda wake.


Akijibu swali hilo bungeni, Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema mkataba huo ulianza kutekelezwa mwezi Julai 2004 kwa muda wa miaka 20 na ulifikia ukomo mwezi Julai 2024.



Amesema mkataba huo ulihusisha ujenzi wa miundombinu ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia kutoka Songo Songo hadi Dar es Salaam pamoja na mitambo ya kufua umeme katika eneo la Ubungo.


Makamba ameeleza kuwa baada ya kumalizika kwa mkataba huo, Serikali ilitoa nyongeza ya muda wa miezi mitatu ili kuwezesha kukamilika kwa majadiliano ya kuongeza muda wa mkataba huo kwa masharti yatakayozingatia maslahi ya pande zote.



Hata hivyo, amesema majadiliano hayo hayakufanikiwa kufikia mwafaka wa kuongezwa kwa muda wa mkataba huo.

Post a Comment

Previous Post Next Post