Na Amini Nyaungo
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari amesema kuwa jopo la wanasheria waliofika Mkoani Singida watasaidia wananchi mbalimbali watakaokuwa na shidaa za kisheria kwa siku saba ambapo leo ndio ulikuwa uzinduzi wake Stendi ya zamani Mkoani Singida.
Hayo ameyasema leo katika uzinduzi wa Kisheria uliofanyika Stendi ya zamani ya Mabasi Mkoani hapa.
Katika hotuba yake Mhe.
Hamza amewataka wananchi kutumia vizuri siku saba ili waweze kunufaika kwa
kutatua shida mbalimbali za kisheria zinazowasibu.
“Niwaase watumie vizuri
siku hizi Mwanasheria Mkuu wa Serikali yupo muitumie vizuri, ambapo hii inafanyika
bure,” Hamza
Aidha Mwanasheria Mkuu wa
Serikali amesema kuwa baada ya uzinduzi wa kamati hiyo utafuatiwa na Kliniki ya
sheria kuanzia leo (Mei 19,05,2025 hadi 25,05,2025)
kutakuwa na huduma za kisheria zitatolewa
kwa wananchi bila malipo yoyote.
Amesema kliniki hizo za
kisheria zinaratibiwa na kusimamiwa na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni utekelezaji wa ibara ya 8 ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo
inaeleza jukumu la serikali la kuwajibika kwa wananchi.
Pia amesema kuwa huo ni
utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia
Suluhu Hassan ambapo amekuwa akiwaeleza viongozi mbalimbali katika kutatua kero
za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Katika kliniki hizo
zitalenga mambo kadhaa ambayo ni pamoja na Kusogeza huduma za kisheria karibu
na wananchi,kuwaongoza wananchi katika taratibu za kupata haki zao pale zinapovunjwa
pamoja na kutoa elimu ya kisheria kwa
wananchi na kuongeza ushrikiano.
Kwa upande wa mgeni rasmi
ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego yeye amezindua rasmi
Kamati ya Ushauri wa Kisheria ngazi ya mkoa na wilaya pamoja na kliniki ya
sheria bila malipo kwa wananchi.
Amesema kuwa “ mpango huu
unalenga kusaidia wananchi wenye changamoto mbalimbali za kisheria kwa
kuwapatia msaada wa kitaalamu bila gharama kama ambavyo Serikali ya Awamu ya
Sita chini ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan imekuwa ikielekeza,” Dendego
Mwisho

Post a Comment