MAFUNZO SHERIA YA PAROLE YATOLEWA MKOANI SINGIDA

 

Na SGT Sophia  Daniely- Singida



Sekretarieti ya bodi ya taifa  ya Parole, ikiongozwa na  Kamishna Msaidizi  Mwandamizi  wa Magereza  ( SACP )Lipiana Lyilo Januari 30,2026 imetoa  mafunzo ya elimu ya Sheria  ya Parole Mkoa wa singida,Maafisa Parole wa ngazi ya Wilaya pamoja  na wakuu wa Magereza Mkoani humo.



Akizungumza  katika mafunzo hayo,SACP Lyimo alieleza taratibu na  vigezo vya  utekelezaji wa Sheria  ya Parole  kuanzia ngazi ya kituo hadi taifa, akisisitiza  umuhimu wa  haki na uwazi katika upatikanaji wa  wanufaika wa Parole.



Kwa upande wake , Mwenyekiti wa bodi ya parole Mkoa wa singida Bw  Liana Hassan, ameshukuru ujio wa sekretarieti ya bodi ya parole taifa umewezesha bodi ya mkoa kutembelea wanufaika wa Parole na kujionea  mabadiliko chanja ya  kitabia.



 Nae katibu wa parole Mkoa wa  Singida , Kamishna  Msaidizi   Mwandamizi wa   Magereza(  SACP) Khatibu Juma Semzono amesema    mafunzo hayo  yataongeza  uelewa  na ufanisi wa utekelezaji wa Sheria ya Parole  kwa wajumbe  na watendaji wa Parole ngazi ya mkoa na  wilaya.



 Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea  uwezo wajumbe  wa bodi ya  parole Mkoa, wakuu wa magereza na  maafisa parole, Pamoja na kubaini changamoto zinazowakabili katika  utendaji wa Majukumu yao.


Mwisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post