WAZAZI/ WALEZI TAMBUENI WAJIBU WENU KATIKA KULEA WATOTO – ASP MDENDEMI


 Na Sylvester Richard



Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Singida, ASP Theresia Mdendemi, ametoa wito kwa wazazi na walezi kutambua na kutekeleza wajibu wao ipasavyo katika malezi ya watoto, ili kuhakikisha wanakua kimwili, kiakili na kiroho.



Ametoa kauli hiyo Januari 12, 2026, wakati akitoa elimu ya ulinzi na usalama kwa waumini wa Kanisa la Anglikana Singida, ambapo alisisitiza kuwa malezi bora ni msingi wa jamii salama na yenye maadili.



Katika maelezo yake, ASP Mdendemi alifafanua kuwa malezi ya kimwili yanahusisha lishe bora na huduma za afya kwa watoto, wakati malezi ya kiakili ni kuhakikisha mtoto anapata haki ya elimu bila vikwazo. Vilevile, alihimiza juu ya umuhimu wa kuwalea watoto kiroho kwa kuhakikisha wanapata mafunzo ya kiimani na kuhudhuria ibada kwa ajili ya kujifunza maadili mema.



Aidha, aliwataka waumini wa kanisa hilo kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa mapema kuhusu viashiria vyovyote vya ukatili au unyanyasaji dhidi ya watoto, ili hatua stahiki zichukuliwe na madhara kwa watoto na jamii kwa ujumla yazuiwe mapema.

Post a Comment

Previous Post Next Post