KAULI ZA LISSU NA MBOWE BAADA YA UCHGAUZI

 

Na Amini Nyaungo
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamemchagua Tundu Anthipas Lissu kuwa Mwenyekiti wa chama hicho katika uchaguzi uliofanyika tarehe (21, Januari 2025) na kutamatika leo.

Hizi hapa ni kuali za Lissu wakati anaongea kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe na kauli za Mbowe baada ya kushindwa uchaguzi.
"Nishukuru Mwenyekiti wetu, tumefanya kitu ambacho haijawahi kufanyika, Mheshimiwa Mwenyekiti uliyestaafu wewe ni Mjumbe wa kamati kuu wa kudumu wa CHADEMA," Lissu

"Tumeweka kiwango kikubwa cha Demokrasia vyama vingine vitufikie wanatakiwa waige kutokea hapa katika chama chetu," Lissu

"Kila aliyelekuwa na haki ya kupiga kura amepiga,"

"Mwenyekiti umefanya kitendo cha busara sana kukubali matokeo kabla ya kufika hapa ni kitendo cha busara sana," 
"Tumefanya uchaguzi wa haki, huru na wawazi, tumefanya uchaguzi uliofuatiliwa na watu wengi waliofuatilia ndani na nje ya nchi,"

"Yote hii tumshukuru Mwenyekiti wetu alifanya hivi kuweka mambo sawa,"
"Mbowe amekipeleka kuwa chama kikuu cha upinzani,"

KAULI ZA MBOWE 

"Ushauri wangu kwenu ushindi wa chama chetu ni ushindi wa wote, ushindi huu usije ukaleta kuvimba kwa walioshinda," Mbowe

"Tembeeni katika katiba ya chama wakati wote kijengeni chama chenu kwa katiba yetu," Mbowe 

"Nilisema uchaguzi huu utaacha majeraha mengi kwa wengi, watu wakasameheane maisha mengine yaendelee," Mbowe.

"Nawaomba ushirikiano i chama kiende mbele," 

Post a Comment

Previous Post Next Post