KAGAME, MUSEVEN WAHUSIKA MGOGORO WA KONGO

Na Amini Nyaungo

PICHA YA MOBUTU SESE SEKO 

Mgogoro wa majimbo mawili ya Mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo unachagizwa na nchi ya Uganda pamoja na Rwanda kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa kupitia Baraza la ulinzi wamethibitisha hivyo na kwenda mbali zaidi kuwa kikwazo kikubwa cha mgogoro huu ni Rwanda na Rais Paul Kagame.

Mgogoro huu umeanzia mbali hadi kufikia leo watu wanajua mapigano makali kati ya M23 na jeshi la Kongo ila hawajui wapi ulipoanza hadi kufikia leo sasa kupitia makala hii utapata kujua M23 ni kitu gani kilianza mwaka gani nani alikianzisha lakini Rwanda, Burundi , Kabila wote wanahusikaje.

March 23,2012 ndio kuanzishwa kwa kundi hili hatari kabisa linaloivuruga Kongo katika machafuko yanayoendelea na wakaita M23, stori ya M23 ipo chini upate historia yake endelea kufuatilia makala hii

TUANZE KIINI CHA MGOGORO HUU NI KIPI ?

Baada ya unyama aliokuwa anaufanya General Joseph Desire Mobutu Sese Seko Kuku wa ZABANGA alitawala Kongo kuanzia mwaka 1965 hadi 1997 alipofariki lakini Kabila alifanimiwa kumuondoa na kwenda uhamishoni.

Mobutu alikuwakatili sana na kuwaua raia mbalimbali historia inasema aliwaonea sana watu wa mashariki mwa Kongo ambapo wapo Watusi kutoka Rwanda na huko ndiko kuna mikoa maarufu ya Kivu Kaskazini mji mkuu wake ni GOMA huku Kivu ya Kusini mji mkuu wake Bukivu na eneo hili ndio kuna madini maarufu sana ya NIKEL na utajiri mwingine.

Baada ya kuona uonevu unaoendelea huko Mashariki mwa Kongo ndipo Laurent Kabila ambaye aliishi sana Tanzania na alikuwa anataka madaraka aliomba usaidizi kutoka katika nchi ya Uganda chini ya Yoweri Museven na Paul Kagame ambapo Kagame wakati huo aikuwa katika majeshi ya Rwanda kabla ya mwaka 2000 kuingia madarakani akiwa Rais wa Rwanda na kuendeleza harakati.

Baada ya Kabila kuketi na viongozi wa Uganda na Rwanda wakatengeneza mkataba ambao umefahamika kwa jina la “Oparation iliyoitwa BANYAMULENGE’ hawa Banyamulenge kihistoria ni kabila la Watusi lililotoka Rwanda karne ya 19 liliingia Kongo mashariki na kuweka makazi yake, sasa hiyo oparesheni iliitwa jina hilo.

Sasa katika makubaliano  kati ya Uganda na Rwanda pamoja na Kabila anapoingia madarakani kutoa haki sawa kwa Watusi au hao Banyamulenge wa Kivu Mashariki lakini pia kuwachukua baadhi ya wanajeshi kutoka Uganda na Rwanda.

Kama ambavyo nilisema huko juu mikoa hii miwili yaani Kivu Kaskazini makao makuu yake Goma na Kivu Kusini Makao makuu yake Bukavu yana utajiri sana mbele utakuja kuona namna gani watu wa Ulaya wanavyosimamia hii shoo ili vita visiishe.

BAADA YA KABILA KUINGIA MADARAKANI

Laurent Desire Kabila alichukua nchi mwezi Mei 17, 1997 baada ya kufanikiwa kumuondoa Mobutu na aliongoza hadi 2001 alipopigwa risasi  na mlinzi wake ambaye alikuwa kabila la Watusi hapa alijichanganganya.

Moja ya mambo makubwa ya kimkataba ambayo nimeyataja, Kabila achukue Wanajeshi kutoka Uganda na Rwanda, Watusi waishi Kongo bila bughudha pamoja na Banyamulenge walindwe kwa hali na mali.

Katika uongozi wake alisahau makubaliano yote waliyofanya na washirika wake na kuanza kuongoza anavyojua ndipo wakaanzisha vuguvugu la yeye pia kuondolewa madarakani .

Waganda na Rwanda waliunda oparesheni nyingine ambayo imeitwa ‘OPARESHENI KITONA’  Kuanzia mwaka 1998 hii iliishia mwaka 2003 ambapo 2001 walifanikiwa kumuua kabisa Kabila .

Ndipo mtoto wake Joseph Kabila kuliongoza taifa hilo kuanzia mwaka 2001 hadi 2019 zaidi ya miaka 18 alidumu madarakani.

Naye hakuweza kufuata matakwa na wale wajomba wa Uganda na Rwanda ndipo mwaka 2009 ilianzishwa oparesheni nyingine ambayo iliitwa CNDP waasi na kiongozi akiwa Laurent Mkunda Batwale lengo lilikuwa pale pale kutetea haki za Watusi ambao wanatesa huko kivu na Goma.

KUANZISHWA  KWA M23

March 23,2012 ndio kuanzishwa kwa kundi hili hatari kabisa linaloivuruga Kongo katika machafuko yanayoendelea na wakaita M23 kifupi vuguvugu lake limeanza mwaka huo.

Hii ilitokaana na wanajeshi waandamizi Bosco Mtaganda na Sultan Makenga kujiengua na jeshi la Kongo kujiunga na M23.

Lengo la M23 kuikumbusha serikali ya Kongo kuwa kulikuwa na makubaliano huko nyuma na hamjayatekeleza mnaendelea kuwaumiza Watusi na sisi sasa tunaingia msituni.

M23 wamechukua udhibiti maeneo ya Rushulu, Rusisi na Benanga ambapo hapo kuna kitivo cha utajiri.

Hii sasa ndio inawaumiza kichwa sana Wakongo maana hawaelewi la kuambiwa wao kusonga mbele kwa mbele.

ULAYA NA AMERIKA WANAINGIAJE ?

Kutokana na utajiri ambao upo maeneo hayo hawa wadwanzi hawakubali kabisa huu mgogoro umalizike maana wanafaida nao wana iba sana mali kutokea hapo hakuna utaratibu mzuri madini yanatorosha na malori huwa yanapita huko huko Kivu.

Ukitaka kushangaa zaidi silaha mpya ya kisasa unaiona huko Marekani na nchi za ulaya keshokutwa unaiona kwa Waasi wa M23 unadhani nani yupo nyuma ya hawa watu kama sio hao wadwanzi ?

Unaweza ukajiuliza kwanini mbona wanatoa misaada ya kiutu  “ Sehemu yoyote ukiona kuna utulivu ujue wajomba wananyonya  au nchi imeamua kuwa "Win win situation” kwamba wawekezaji wananufaika na nchi husika inanufaika.

Kagamne mara kadhaa ameulizwa juu ya kuhusika na mgogoro huu amekuwa akikataa lakini waliothibitisha tayari nimekwamba UN katika Baraza la Ulinzi limeweka bayana hilo kuwa Rwanda wanahusika kwa kiwango kikubwa sana.

Rais wa Angola Joao Lourenco aliwahi kuwaita Tshekedi na Kagame akawa mzito katika hili na kuna namna ya ugumu anauweka huyu jamaa wetu.

KWANINI MAGONJWA MENGI YA MLIPUKO CONGO?

Uliwahi kujiuliza kwanini magonjwa mengi yanaanzia Kongo kisha yanaenda sehemu nyingine ? basi kama ulikuwa hujui Kongo ndio sehemu ya Wanasayansi kufanya majaribio ya utafiti wao wa magonjwa mbalimbali hivyo ni rahisi kuingiza ajenda zao kwa watu wa kongo.

Fikiria, Marburg, Corona ilianzia Ulaya lakini kwa Afrika ilianzia hapo , MPOX na mengine mengi wazungu sio watu wazuri wanachukulia machafuko kuingiza mambo yao.

MAONI YANGU

Nafikiri umoja wa Afrika Mashariki unatakiwa kuwatenga Uganda, Kongo na Rwanda pia umoja wa Afrika nao wangefanya hivyo ili kila kitu kikae sawa wakikaa wenyewe huenda watabadilika.

Mgogoro huu bila ya kujitambua hauwezi kuisha maana yupo mtu wa tatu anayeingiza ajenda zake huyu anatakiwa aondoke na utulivu ubakie. Vinginevyo kila siku tasikia tu mapigano na hayatofika mwisho ukibisha kaa hapo hapo lakini hili jambo nyeti sana kwa watu wa Uaya katika shabaha zao za mali ambazo zinapatikana Kongo lazima watu wawavumbue akili zao viongozi wa Kongo na M23 na makundi mengine yanayo sababisha vurugu hapo Kongo vinginevyo maji yatatwangwa katika kinu na hakutokuwa na muafaka wa kudumu ndani ya nchi hzi za Afrika ikiongozwa na KONGO. 

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post