DR SLAA CHANZO CHA LOWASA KUINGIA CHADEMA


Na Amini Nyaungo
Imeelezwa kuwa kujiunga kwa aliyekuwa mgombea Urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Edward Lowasa mwaka 2015 aliyemshawishi ni Dokta Willibrod Slaa ambapo wakati huo alikuwa Katibu Mkuu wa chama hicho.

Hayo yamesemwa jana (Januari 16,2025)na Tundu Antipas Lissu wakati wa mdahalo ambao umeandaliwa na kituo cha habari cha Star TV wa kutoa sera katika kugombea nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA, ambapo walialikwa wagombea wote watatu , Odero, Mbowe na Lissu na waliotokea ni wawili Edero na Lissu.
Lissu ameweka bayana kuwa ushawishi na vikao vyote vya kumtoa Lowasa Chama Cha Mapinduzi(CCM) lilikuwa wazo la Dokta Slaa ambaye aliwashawishi viongozi wa ndani ya chama hicho na wakakubali ila yeye(Lissu) na Mnyika walipata taarifa hizo kwa kuchelewa maana hawakuwa wanataka aingie ndani ya CHADEMA.

" Mchakato wa kumleta Lowasa ndani ya Chama Chetu aliuanzisha Dokta Slaa amefanya vikao vyote na kusimamia hadi ujio wake ndani ya CHADEMA,"Lissu.

Aidha, Lissu baada ya mchakato kukamilika alishangaa kumuona Dokta Slaa akiondoka CHADEMA kwa kigezo cha kutokukubaliana na ujio wa Lowasa wakati mchakato wote aliufanya yeye.
"Nimeshangaa sana kuona Dokta Slaa anakaa pembeni wakati yeye ndiye aliyehusika kuwashawishi viongozi kumleta Lowasa,"ameongeza

Katika mdahalo huo Lissu aliulizwa juu ya kuhama ndani ya CHADEMA  kama akishindwa uchaguzi amejibu kuwa hawezi kuhama na atampongeza Mbowe kama atashinda lakini ashinde kwa haki na kusiwe na wizi wa kura na mambo mengine.
"Hahami mtu hapa, aliyeuliza juu ya kuhama  mimi nipo na naona kila kitu kipo upande wangu hivyo sihami, nitampongeza atakayeshinda kama uchaguzi hautokuwa wa rushwa na mambo mengine machafu nitampa mkono na tutaendelea kukijenga chama,"Lissu

Katika sera zake endapo atapata ridhaa ya kuongoza CHADEMA akiwa Mwenyekiti atarekebisha mifumo ya ndani ya chama hicho kuwa na muungano na wazi, lakini pia amesimamia katika msimamo wa kutokuwa na maamuzi mawili kwa wakati mmoja.
Atapambana kuzuia maswala ya rushwa ndani ya chama hicho na utawala bora wenye mabadiliko  na kusisitiza kuwa kuelekea uchaguzi mkuu endapo hakuna mfumo sahihi wa wasimamizi wa ypigaji kura hakutokuwa na uchaguzi.

Mwisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post