Na Charles Kikoricho, Singida
Afisa lishe halmashauri ya Wilaya ya Singida Edes Tarimo amewaomba wananchi wajitokeze katika vituo vya afya vilivyopo karibu kwaajili ya kupata Matone ya Vitami A , dawa za Minyoona upimaji au ufanyikaji wa Tathimini ya hali ya lishe kwa watoto nchini ya umri wa miaka mitano.
Afisa lishe Ndugu Edes Tarimo amesema hayo leo tarehe 19.12.2024 katika kipindi cha Zinduka kinachorushwa na Standard Radio na kuwaomba wazazi na walezi watumie mwezi huu wa afya na lishe kwa watoto kwa kuwapatia haki yao ya msingi kwa kuwapeleka kwenye vituo vya afya vilivyopo katika maeneo yao ili waweze kupatiwa huduma za kufanyiwa tathimini ya hali ya lishe na kupata dawa za minyoo pamoja na matone ya Vitamini AMwezi wa Afya na Lishe kwa watoto chini ya miaka mitano imekuwa ni utaratibu unaofanyika kila mwaka ifikapo mwezi wa kumi na mbili na mwezi wa sita na zoezi hili huambatana huduma za utoaji wa matone ya vitamini A ,dawa za minyoo na kufanya tathimini ya hali ya lishe kwa watoto wote walio na umri wa kuanzia miezi 6 hadi miaka 5.
Post a Comment