Na Ofisi ya Mufti
Aliyekuwa katibu wa BAKWATA mkoa wa Singida Alhaj Burhani Amri Mlau aliyefahamika sana huko nyuma kwa "Lakabu" ya Katibu kiongozi ambaye sasa amepandishwa na kuwa afisa msaidizi ofisi ya Katibu Mkuu BAKWATA makao Makuu leo amemkabidhi ofisi katibu mpya wa mkoa huo alhaj Omar Muna ambaye kabla ya uteuzi wa wiki hii alikuwa katibu wa BAKWATA mkoa wa KataviMakabidhiano hayo yamefanyika mapema leo mbele ya maafisa wa BAKWATA mkoa huo ikiwa ni pamoja na mjumbe wa Halmashauri Kuu BAKWATA anayewakilisha mkoa wa Singida alhaj Juma Kilimba, Qadhi wa mkoa sheikh Ramadhani Kaoja almukarram, mratibu wa elimu na viongozi wa JUWAKITA na JUVIKIBA mkoa huo.
Akiongea baada ya makabidhiano hayo alhaj Burhan bin sheikh Mohammed bin Sheikh Amri Mlau amewashukura sana viongozi wa BAKWATA na waislamu wote wa mkoa huo kwa ushirikiano mkubwa waliompa muda wote wa miaka ishirini na tano tangu alipokuwa katibu wa ujenzi Masjid Taq-wa, katibu wa kata ya Ipembe, mhasibu wa wilaya ya Singida mjini, mhasibu mkoa wa Singida na kubwa zaidi ni ushirikiano mkubwa sana waliompa miaka kumi na moja akiwa katibu wa mkoa huo.
Aidha alhaj Burhani Mlau amewashukuru sana viongozi wa serikali ngazi zote mkoa huo na viongozi wa Taasisi mbalimbali za kiislamu wa madhehebu yote mjoa huo pamoja na wananchi wote wa mkoa huo kwa sababu amesema ushirikiano huo umemjengea heshima kubwa na kuendelea kuaminika ndani na nje ya mkoa huo na hasa mbele ya Mh. Mufti Dr. Abubakar Zubeir, Katibu Mkuu Alhaj Nuhu Mruma na viongozi wote BAKWATA makao makuu.
"Walionishauri muda huu wote nawashukuru sana pamoja na wale walioendelea kuniombea Mungu Allah awalipe kila la heri duniani na akhera. Familia yangu nayo Allah awalipe kwa uvumilivu wao mkubwa muda wote ninapokuwa mbali nao kutekeleza majukumh yangu" Amesema alhaj Mlau.
Alhaj Burhan ataripoti ofisi ya katibu mkuu BAKWATA mapema wiki ijao mara tu baada ya hafla kubwa iliyoandaliwa na waislamu wa mkoa huo kumpongeza kwa wadhiufa mpya na kumuaga.
......
Dr. Harith Nkussa
Msemaji Maalum wa Mufti
Alhamisi 19.12.2024
Bolisa. Kondoa.
Post a Comment