Na Amini Nyaungo
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Singida Vijijini Shabani Mang'hola ametambua mchango wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Martha Mlata na Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego kwa kuendelea kufanyakazi vizuri.
Mang'hola ameyasema hayo leo Standard Radio akithibitisha juu ya uchapaji kazi wa Mwenyekiti wa CCM ndugu Martha Mlata akimuelezea kuwa moja ya watu muhimu kwani anaunganisha chama pamoja na uzalendo."Mlata ni mtu muhimu sana katika mkoa wetu wa Singida anatuunganisha vyema tuna umoja ndani ya Chama Cha Mapinduzi, mimi binafsi najifunza mengi kutoka kwake, tumpe ushirikiano," Mang'hola
Aidha ameweka wazi kuwa Mlata ni mtu muhimu sana katika ushindi wa CCM akisema kuwa kuuanganisha umoja kwa Wanachama.Kwa upande wa mkuu wa mkoa amesema kuwa utendaji wake wa kazi pamoja na mipangilio mizuri ya kusimamia miradi.
"Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego anafanyakazi nzuri sana anatufanyia kazi ndani ya chama iwe rahisi kwa kusimamia miradi ya maendeleo vizuri na pesa zinazoletwa na Rais Samia," Mang'hola
Pia ametumia fursa hiyo kuwashukuru Wanachama wa CCM kwa kuwachagua katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa kura nyingi na za kishindo." Nawashukuru sana Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kwa kutuchagulia wenyeviti wa CCM na wajumbe wanaotoka katika chama chetu," Ameongeza
Mwisho.
Post a Comment