HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » SILAA- IGHONDO MTU BWANA ANAPAMBAIA JIMBO LAKE, AZINDUA SHULE YA BILIOMI MOJA

 

Na Amini Nyaungo
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa ameweka ampongeza Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Ramadhan Ighondo kwa kazi nzuri anayoifanya katika Jimbo hilo.

Silaa hayo jana tarehe 25.10.2024 Makuro mkoani hapa ambapo amesema kuwa Ighondo amekuwa akilipambania Jimbo lake kwa kuyasemea mambo mbalimbali ya maendeleo ili Wananchi wake waishi katika vizuri.
Silaa amesema kuwa katika minara 33 ya Mkoa wa Singida mimara 8 ipo katika Jimbo lake la Singida Kaskazini.
Aidha amebainisha kuwa wakati anakuja amemdokeza juu ya sehemu ambazo mtandao wa simu haupatikani hivyo kupitia minara hiyo hivi punde wananchi wa Singida Kaskazini watapata mawasiliano na Jimbo hilo litakuwa la kisasa zaidi.
"Ndugu zanvu mmepata Mbunge Jembe mno, Ighondo anapambania Jimbo lake hata wakati nakuja huku tulikuwa tunawasiliana, katika minara 33 ya mkoa wa Singida jimbo hili limepata minara 8, na sehemu ambazo mtandao unasuasua tatizo hilo litaisha hivi punde tu na jimbo litakuwa safi kabisa," Silaa

Shule hiyo mpya iliyojengwa imelenga kupunguza msongamano mkubwa wa wanafunzi katika shule ya sekondari Ilongero na kuwapunguzia adha wanafunzi kutembea umbali mrefu baadhi ya wanafunzi waliokua wakisoma shule ya Sekondari Ilongero imezinduliwa rasmi leo Oktoba 25, 2024.

Akizungumza maara baada ya kukagua majengo na kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo Waziri Silaa amesema hiyo ni sehemu tu ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya elimu nchi nzima ikiwa ni pamoja na Mkoa wa singida.

Ametoa rai kwa wanafunzi wa shule hiyo mpya iliyoanza rasmi januari 2023 ikiwa na idadi ya wanafunzi 483 hadi sasa kuhakikisha wanasoma kwa bidii kwa kuwa tayari Serikali imeweka miundombinu bora katika shule hiyo.

Akitoa taarifa ya Mradi wa shule hiyo Mkuu wa Shule ya Sekondari Sekoutoure Tatu Njaku amesema ujenzi wa shule hiyo umeboresha mazingira ya Kufundishia na wanafunzi kujifunza.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego kwa ujumla wake amesema kwa kipindi cha miaka Mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,Mkoa wa Singida unashule mpya za sekondari 33 ikiwa ni kuendelea kupunguza changamoto za wanafunzi kusoma umbali mrefu.
Mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply