Na Amini Nyaungo
Mbunge wa Singida Kaskazini Ramadhan Ighondo amesema ujio wa makocha kutoka nchi ya Sweden unaweza kuleta chachu ya vijana kupenda mpira pamoja na kujipatia ajira hapo baadae baada ya kupata mafunzo.
Hayo ameyasema leo wakati wa Kliniki ya kufundisha watoto "Grassroots" ambayo imefanyika Ilongero Halmashauri ya Singida Vijijini ndani ya Jimbo la Singida Kaskazini ambalo analiongoza Ighondo.
Makocha hao amewaleta Ighondo akiwa na lengo la kuwakumbusha wazazi kuwa mtoto anatakiwa apate fursa kama ana kipaji cha kucheza mpira.
"Nimewaleta hawa ili watoto wetu wapate mafunzo ya mpira wakiwa watoto na naamini wakiweza huko baadae watasajiliwa na timu kubwa watatimiza malengo yao ya kucheza mpira hatimaye kupata ajira,"Ighondo
Katika kliniki hiyo sio tu wanafunzi bali makocha zaidi ya 80 wamepata mafunzo ya ukocha wa vijana na kuwanufaisha katika vituo vyao mbalimbali.
Licha ya hayo Ighondo pia amesema anamuunga mkono Rais Samia katika michezo kwani yeye anawaleta makocha ili Singida wapate timu nzuri ambapo wataisaidia Tanzania na kutangaza nchi kama ambavyo Rais Samia anafanya.
Ighondo anasema kuwa lengo la hamasa kwa Rais Samia kununua goli ni kuhamasisha mpira kukua lakini pia timu inapofanya vizuri inaitangaza nchi.
"Watu inawezekana hawajui ila lengo la Samia kutangaza nchi pamoja na kuhamasisha michezo kukua, namie natumia nafasi hiyo kukuza michezo kwa kuwaletea makocha ili hawa wachezaji baadae waje watangaze nchi yetu kwa kupambania bendera ya taifa," Ighondo.
Kesho tarehe 30.10.2024 makocha hao watakuwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida kwa ajili ya kuwafundisha makocha wa mkoa wa Singida, lakini pia baada ya hapo wataenda katika sehemu mbalimbali ndani ya Jimbo la Singida Kaskazini.
Mwisho.
No comments: