Ogbunuju amesema hayo leo akibainisha lengo kuu la kituo cha Faraja kuona watu mbalimbali wanafanikiwa kiuchumi ili wazisaidie familia zao, ndio maana leo wametoa vifaa hivyo.
"Leo ndio siku ambayo Mungu ameipanga tukutane, lengo letu kuona kila familia inafanikiwa tumepata hivi vifaa viwasaidie kujiendeleza katika biashara zenu," Ogbunuju.
Katika hatua nyingine amewaomba wote waliopata usaidizi wa vifaa walivyopewa wakavitumie vizuri na wakifanyie maendeleo ili waje wawainue wengine.
"Tumetoa vifaa hivi mkavitumie vizuri ili vije kuwasaidia wengine katika familia zenu, vitunzeni na mvifanye vizalishe.
Katika zoezi hilo la kuwakabidhi Ogbunuju ametoa vifaa mbalimbali kwa vikundi 16 vya aina tofauti ikiwemo vikundi vya Umwagiliaji, Ushonaji, Wafugaji wa Nyuki, Wapambaji pamoja na Ufugaji wa Kuku.
Aidha kwa upande mwingine waliopata kupokea vifaa hivyo wamefurahishwa na kuwaomba waendelee kuwasaidia wengine.
Mohamed Omary maarufu kama "Majengo Nyuki" yeye amesema kuwa kituo cha Faraja cha Mkoani Singida kinaendelea kuwaneemesha kwa kutoa misaada ya aina tofauti kuwasaidia Watanzania.
"Hiki kituo cha faraja wanajitahidi sana kutusaidia waendelee hivi hivi naamini tutafanikiwa, niwaombe wote waliopata hio fursa leo waiendeleze,"Amesema.
Asante Mfuatiliaji wa Chamber Media Ukiwa na Maoni au Jambo lolote Kuhusu Taarifa Zetu Tafadhali Wasiliana nasi +255 717 519 981 Asante na Endelea Kubaki nasi..
No comments: