Na Mwandishi Wetu Dodoma
Mamlaka za Udhibiti kutoka Angola, Botswana, Afrika Kusini, Namibia, Lesotho, Eswatini, Zambia, Malawi, Msumbiji, Zimbabwe na Tanzania zimeshiriki vikao hivyo. Kwa upande wa Zanzibar, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA) imeshiriki kama mtazamaji kwa kuwa bado haijawa mwanachama wa umoja huo.
Vikao hivyo vitakavyofanyika kwa awamu mbili, kati ya tarehe 23-27 Septemba, na 8-11 Oktoba, 2024, vinajadili pamoja na mambo mengine, namna ya kuboresha shughuli za udhibiti wa nishati katika maeneo ya fedha, rasilimali watu, huduma kwa wateja, habari, mawasiliano na teknolojia ya habari. Masuala mengine ni kuhusu udhibiti kiufundi na kiuchumi ikijumuisha bei, tozo na viwango vya huduma kwenye sekta za umeme.
No comments: