Na Amini Nyaungo
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Singida Jesca Kishoa amekabidhi kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya mabati ya kuezeka soko la bidhaa mbalimbali la Gumanga wilaya ya Mkalama mkoani hapa.
Soko hilo limekuwa limeezekwa kwa nyasi huku wafanyabiashara wa eneo hilo wakiendelea na shughuli zao ziara hiyo ya Kishoa imekuwa kama tiba ya kuanza safari mpya ya soko la Gumanga.
Hayo yamefanyika leo katika ziara ya Mbuge huyo alipotembelea hapo na kutaka kujua kero mbalimbali za wananchi aneo hilo na kuongea nao wananchi wengi walikusanyika huku fedha hizo amemkabidhi Mwenyekiti wa soko hilo aliyefahamika kwa jina la Aisha.
Soko hilo linazaidi ya miaka 30 linawasaidia wananchi wa eneo hilo kwa kuuza bidhaa mbalimbali ambapo wamemuomba Kishoa awasaidie ili liwe la kisasa na ameweza kuwajibu hapo hapo kwa kiasi hicho cha pesa.
Aidha katika hatua nyingine Kishoa amewaomba wananchi wajitokeze kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili watumie haki yao ya msingi ya kupiga kura.
Mwisho.
No comments: