Na Amini Nyaungo
Vijana
wametakiwa kuwa wamoja na kulinda amani ya nchi ya Tanzania kwa kuungana kwa
pamoja ili waimarishe undugu pamoja na vuguvugu la kujitolea ii kuleta
mapinduzi ya kifikra kwa jamii pamoja na kuhimizana fursa mbalimbali katika
jamii.
Hayo
ameyasema leo Katibu wa Taifa letu Kesho yetu Movement maarufu kama (TK Movement)
Zanura Adam walipokuwa wanazindua kampeni hiyo kata ya Merya Mkoa wa Singida
ambapo mgeni rasmi alikuwa Diwani wa kata hiyo Iddi Rajabu akimuwakilisha
Mwenyekiti wa CCM Halmashauri ya Mnaipsaa ya Singida Vijijini Elia Digha.
“TK Movement ipo kwa ajili ya kuleta mapinduzi ya kifikra katika jamii, haifungamani na mtu yoyote, dini, chama au kabila,”Zanura
Zanura
amewaomba vijana kuungana na TK Movement ili waweze kuwa pamoja , amesema
kitaifa ilizinduliwa tarehe 25.05.2024 huku kwa mkoa wa Singida ilizinduliwa
tarehe 20.07.2024 kwa upand wa wilaya ya
Singida vijijini imezinduliwa 31.08.2024 leo hii wamezindua katika kata ya
Merya.
Kwa upande wake mgeni rasmi wa tukio hilo Diwani wa kata ya Merya Iddi Rajabu amewaomba vijana kubadili na kumrudia Mungu ili kuweza kuondoa mambo ya ajabu yanayoendelea hapa nchini.
Rajabu
amesema ni lazima vijana wawe tayari kubadilika na kuwa na hofu ya Mungu ili
kila kitu kiwe katika mstari uliokuwa mzuri.
Mwisho
No comments: