HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » KITILA AREJEA SIREFA, YAGI AWEKA MIPANGO


Na Amini Nyaungo
Mwenyekiti wa  Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida Hamis Kitila amerejea madarakani baada kipindi chake cha miaka minne  kumalizika na kuomba tenà kura na wajumbe wamempa kura zote na kurudi tena kuongoza mpira wa mkoa wa Singida.

Uchaguzi huo umefanyika leo tarehe 17.08.2024 katika ukumbi wa Mkuu mkoa wa Singida ambapo tukio hilo limefanyika ambapo kabla ya kuchaguliwa ilianza na kuzipotia ajenda 15 zilizowekwa na SIREFA kisha ndio uchaguzi umefanyika.

Aidha viongozi kutoka TFF walikuepo kuangalia kile kilochokuwa kinaendelea na kuridhishwa na aina ya uongozi wa mkoa wa Singida.
Katika hatua nyingime Kitila na jopo lake wameweka mipango mikakati ya kupata angalau timu mbili zitakazokuwa zinashiriki ligi kuu ya Tanzania bara (NBC Primer League) kwa msimu wa mwaka 2025/2026

Kitila amesema kwasasa mkoa unafaidika na uwepo wa timu moja iliopo hivyo wanatarajia kuongeza timu nyingine kwaajili ya manufaa zaidi ya kimkoa na shirikisho 

"Tunataka mwakani kupata timu nyingine ya ligi kuu kwa kushirikiana na wadau wengine, kwasasa wananchi wa mkoa wa Singida wanapata burudani lakini pia uchumi unaimarika" 

Singida Black Stars ndio timu pekee kwasasa inayoshiriki ligi kuu kwa mkoa wa Singida mara baada ya kubadilishwa jina kutoka Ihefu baada ya kuhamia kutoka mkoani Mbeya kuja mkoa wa Singida na Singida Fountain Gate kuhamia mkoa wa Manyara na kubadilishwa jina kuwa Fountain Gate fc

Kwa mujibu wa mhasibu wa SIREFA Charles Kimwaga amesema kwa mwaka huu shirikisho limetenga bajeti ya milioni 67 ikiwa na ongezeko la milioni 17 toka bajeti ya mwaka Jana ambayo ni milioni 50

"Kwa mwaka huu tumetenga bajeti ya milioni 67" amesema mhasibu Kimwaga

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida YAGI Maulid KIARATU amesema kuwa ataendelea kusapoti soka la mkoa wa Singida hususami wanawake ambako atawaangalia kama ilivyokuwa kipindi kilichopita.

"Tutaendelea kusaidiana lakini nitasimamia vizuri mpira wa wanawake kwa hali na mali kama ambavyo ilivyokuwa miaka minne.

Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply