Na Amini Nyaungo
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Singida Nusrat Hanje amewataka wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars” kuipambania bendera ya Tanzania kuelekea michuano mikubwa Afrika “AFCON” ambayo inatarajiwa kuanza kuchezwa mwaka 2027 katika ushrikiano wa ardhi ya Tanzania, Kenya na Uganda.Hanje ameyasema hayo alipokuwa anahojiwa na Clouds FM ambao waliandaa mdahalo wa watu mbalimbali kuelezea michezo ndipo akatoa maoni yake.
Amesema kuwa licha ya Serikali ya awamu ya sita kujitahidi kujiandaa katika Miundombinu na mambo menginme ili michuano ikifika iwe katika hali nzuri bado amewataka wapambane uwanjani ili wawape furaha Watanzania.
“Pamoja na kuwa tutajiandaa upande wa Miundombinu na sekta zingine tujitahidi pia uwanjani tusiwe wanyonge,” Hanje.Ameendelea kusema kuwa kwa mtazamo wake katika nchi tatu zilizopewa nafasi ya kuwa wenyeji wa michuano hiyo Tanzania ndio nchi yenye mwamko mkubwa katika soka.
“Katika nchi zote ambazo zita host AFCON 2027 Tanzania ndio mamaster kuanzia muamko na hata maandalizi,” amesema.
Kwa mara ya kwanza nchi za Afrika Mashariki zitakuwa wenyeji wa michuano hii mikubwa Barani Afrika mwaka 2027 ambapo Shirikisho la soka Tanzania, Kenya na Uganda watapata heshima hiyo.mwisho
No comments: