Wakati Teknolojia ikikua kila siku kata ya Mughunga Wilaya ya Singida bado mawasiliano ya simu yanasuasua kwa kukosa mtandao.
Hayo yamesemwa jana katika Baraza la Madiwani iliyofanyika Halmshauri ya wilaya ya Singida aliyetoa taarifa ni diwani wa kata hiyo Hassan Mtinange alipokuwa anawasilisha taarifa yake.
Baada ya taarifa hiyo Mwenyekiti wa Kikao hicho Elia Digha ameomba tàasisi na Mashirika mbalimbali kuwasaidia wananchi hao kwani wanapata taabu ya kupata mawasiliano ya simu.
Digha amesema kuwa wakazi wa eneo hilo wanatembea Kilomita tano hadi kumi kutafuta mtandao wa simu huku wengine wakipanda katika miti ili kuwasiliana na ndugu zao.
"Niombe nyinyi wanahabari pamoja na wadau mbalimbali mtusaidie tupate mnara Mughunga,"Digha.
Asante Mfuatiliaji wa Chamber Media Ukiwa na Maoni au Jambo lolote Kuhusu Taarifa Zetu Tafadhali Wasiliana nasi +255 717 519 981 Asante na Endelea Kubaki nasi..
No comments: