Na Amini Nyaungo
Afisa Habari wa Singida Black Stars Hussein Masanza ameweka wazi kuwa timu hiyo itakuwa mikononi mwa Wanasingida baada ya kurejea katika maandalizi ya msimu ambapo kwa sasa wapo mkoani Arusha.
Masanza amesema watakaporejea katika maandalizi ya timu wataikabidhi kwa Wanasingida ili waendelee kufurahia na kuwa katika sehemu ya timu.
Amewaomba mashabiki wa timu hiyo wafike kwa wingi siku ya tarehe 10 08.2024 katika siku yao ya kutambulisha kikosi chao na benchi la ufundi kutakuwa na mambo mazuri.
Masanza ametanabaisha kuwa timu inaendelea vizuri pamoja na mazoezi ana amini msimu huu unaonaza mwezi wa nane huenda wakaondoka na chochote akiwahakikishia mashabiki wa timu hiyo kuwa watapata ubingwa katika mashindano wanayoshiriki.
"Kwa kikosi tulicho nacho naamini tunaweza kupata ubingwa msimu huu niwaambie mashabiki wa Singida Black Stars wataenda kunyanyua kwapa," Masanza.
Singida Black Stars watafanya tamasha lao kubwa tarehe 10.08.2024 katika uwanja wa Liti kuweza kutambulisha wachezaji wao na benchi la ufundi.
Mwisho.
No comments: