Amini Nyaungo
Mwenyekiti wa Chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Singida (SIREFA) Hamis Kitila leo amefungua ligi ya Chief Thomas Mgunto Siuyu Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Katika uzinduzi huo Kitila amesisitiza vijana kujitoa katika mpira kwani ndio mchezo wenye ajira nzuri, licha ya kupata kipato mchezaji anajiweka katika afya nzuri.
Kitila amewaambia wananchi waliokusanyika eneo hilo ya kuwa kuna baadhi ya wachezaji ambao amewaona wataungana na wengine katika majaribio ya kucheza timu B ya Singida Black Stars.
"Natangaza kuwa leo tumefanya uzinduzi wa ligi hii lakini kuanzia tarehe mbili hadi tarehe nne kutakuwa na majaribio ya vijana waliochini ya mika 20 kwa ajili ya kujiunga na timu ya vijana na Singida Black Stars," Kitila.
Cheif Thomas Mgunto ambaye ndiye muanzilishi na mwenye kombe hilo amesema kuwa kwa sasa ni mwaka wa tatu wameongeza timu na kufikia 20 hivyo wameendelea kutengeneza vipaji vingi vya wachezaji.
"Tumeongeza timu na sasa zimefika 20 tofauti na misimu miwili iliyopita," Mgunto.
Ligi hiyo inahusisha timu 20 ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na milioni moja huku atakayeshika nafasi ya pili atapokea kitita cha shilingi laki tano na wa tatu atapokea laki mbili na nusu.
Mwisho
No comments: