Hayo ameyasema leo Sheikh Tibaijuka hapa Chamber Media ya kuwa sadaka hii inatolewa ili kusafisha funga za mwanadamu na amesema kuwa anayestahili kutoa ni yule kiongozi wa familia.
Tibaijuka amesema kuwa kiasi kinachotakia kutolewa ni kilo tatu ya chakula cha nafaka kinachopendwa eneo husika, kila kichwa kinatolewa kisi hicho amesisitiza kuwa kama hauna kisi hicho anatoa aliyekuwa nauwezo akiomba wasikope na kuiba kama hauna sadaka hiyo.
Ameweka wazi kuwa anayestahili kupata sadaka hiyo ni yule fukara ambaye hana uwezo wa kufurahia siku ya siku kuu ya Eid.
" Dhaka tul fitri atoe yule mwenye nafasi na uwezo kama huna uwezo basi toa ulichonacho Mungu atajua yaliyo moyoni mwako," Tibaijuka
Leo ni Ijumà ya mwisho wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa katika kumi la mwisho la kuachwa huru na moto kwa wale wanaotenda mema.
Mwisho.
Post a Comment