Wananchi katika kijiji cha Manga mkoani Singida wameaswa kumlinda na kumtetea nyuki ili wapate kufaidika naye kwakuwa anafaida kubwa ambapo ukiwa na mizinga ya nyuki yanaweza kukupa pesa nyingi kwa yaliyomo ndani yake elimu hiyo imetolewa leo na Mohamed Omary maarufu kama Majengo Nyuki katika kijiji cha Manga mkoani Singida.
Majengo ameto elimu ya namna maisha ya nyuki na usaidizi wake katika jamii ya Tanzania akitanabaisha kuwa Nyuki ana faida kubwa kwa maisha ya mwanadamu hususani katika maendeleo ya jamii , amesema kuwa kuna Nta, Royal Jery, pamona na Sega, akieleza kuwa Royal Jery inaweza ikakupa mamilioni ya pesa maana inasoko kubwa duniani.
"Nyuki analeta asali, ana chavusha mazao pamoja na kuwa na kinga katika seli za mwanadamu," Majengo
Ametumia fursa hiyo kumuomba mgeni rasmi wa tukio hilo la shamba darasa kuruhusu elimu hiyo itolewe mara kwa mara.
Baada ya tukio hilo Chamber Media imemuuliza juu ya matumizi ya nyuki na yaliyomo amesema kuwa kuna vitu vingi ikiwemo Royal Jery , Nta ambapo kupitia Nta wanaweza kutengeneza mafuta ambayo yanasaidia kutunza ngozi ya manadamu pamoja na kutunza vyuma visipate kutu.
Ameeleza kuwa kutumia supu ya nyuki inaweza ikaimarisha nguvu za kiume pamoja na kuthibiti magonjwa mbalimbali.
Shamba darasa hilo limehudhuliwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa Siasa, viongozi wa SMAUJATA pamoja na wanakijiji wa eneo hilo ikiwa ni kupata elimu hiyo ya umuhimu wa Nyuki.
Mwisho.
Post a Comment