TOENI TAARIFA ZA RUSHWA VIJANA -MWANJALA



Vijana wameshauriwa kutoa taarifa popote wanapoona viashiria vya rushwa pia wasipokee kwani kufanya hivyo ni kosa Kisheria ikibainika itawapelekea kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Hayo yamesemwa leo na  Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU)  mkoa wa Singida  Sipha Mwanjala lililofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Uhasibu(T. I. A) mkoani hapa. 
Mwanjala amewaomba vijana wasisite kutoa taarifa wanapoona viashiria vya rushwa huku akiwaasa wasitoe wala kupokea rushwa. 

Ametumia nafasi hiyo kuweka wazi kuwa wameamua kuwapelekea elimu hiyo kwakuwa vijana wakielewa madhara ya Rushwa wataweza kusambaza elimu  kwa watu wengine. 

"Vijana msisite kutoa taarifa mnapoona viashiria vya rushwa, tumeamua kuwapelekea vijana elimu hii kwani wao wakielewa wataweza kusambaza kwa wengine, " Mwanjala.

Vijana ambao wameshiriki katika kongamano hilo wameaahidi kushirikiana na TAKUKURU Mkoa wa Singida kupinga na kukataza rushwa. 

Mwanafunzi Ezekia Tweve wa Chuo cha Uhasibu Singida amehaidi kuwa, kama kijana atakuwa mstari wa mbele kuwafichua wale wote wanaotoa na kupokea rushwa kwa kushirikiana na TAKUKURU baada ya kupata elimu ya rushwa iliyotolewa kwenye kongamano la vijana wa vyuo Mkoani Singida. 

Lakini pia Afrodina Chrispine Mchele yeye ni mwanafunzi kutoka Chuo cha Maji ameshauri TAKUKURU waendelee kutoa elimu hiyo kwa vijana kwani inawakumbusha wajibu wao huku akiahidi kuwa mstari wa mbele kuzuia na kukataza Rushwa.

Naye Ismail Ayoub ambaye kiongozi wa SKAUTI Manispaa ya Singida ameahidi ushirikiano kwa pande zote mbili pamoja na kuwapa elimu wengine. 

Elimu hiyo imetolewa kwa vyuo vinne ikiwemo Chuo cha Maji, Chuo cha Uhasibu Tawi la Singida, Skauti pamoja na Chuo cha Utumishi. 

Post a Comment

Previous Post Next Post