VIJANA UNGANENI MPATE MIKOPO MJIENDELEZE- NDAHANI

 

Afisa Vijana mkoa wa Singida Fredrick Ndahani amewaomba vijana kuchangamka fursa mbalimbali zinazopatikana mkoani hapa hususani mikopo ya asilimia kumi pamoja na mfuko wa uwezeshaji wa Waziri Mkuu.


Hayo ameyasema leo alipoongea na Standard Radio katika Kipindi cha Zinduka kinachoruka Asubuhi, amesema yakuwa vijana wana fursa nyingi katika kujiletea Maendeleo hivyo wasikae nyumbani wanapoona fursa.

Wakati huo amewaomba vijana kujiunga katika vikundi vya watu kuanzia watano na waonyeshe mradi upi ambao wanaenda kuufanya katika maandiko yao ili iwe rahisi kupata mikopo hiyo.


"Nashauri mnapoomba mikopo muwe na kitu cha kufanya ili muweze kupata mikopo hiyo inyotolewa serikali na mujiendeleze kiuchumi," Amesema.

" Katika wakati huu ambao mikopo inatarajia kurejea watu wajiunge na vikundi mbalimbali ili ikikamilika basi muwe tayari,"Ndahani 

Ndahani ametumia fursa hiyo kutaja idadi ya vijana mkoa wa Singida ambapo ni 541,586 katika idadi hii wanaume 266,999 huku wanawake ikiwa ni 274,599 ikionesha idadi hii ni asilimia 27 ya vijana na hii ni idadi kubwa  kuliko idadi nyingne hivyo wajipange vizuri ili wapate mikopo.


Amesema kwa mwaka uliopita ofisi yake imepata zaidi ya maandiko 50 ambayo yanalenga kupata mikopo katika mfuko wa uwezeshaji wa Waziri Mkuu.

Kutokana na kasi hiyo ya vijana ameomba vijana wajitokeze, lakini pia amewaomba kujiingiza katika maswala ya uongozi hususani chaguzi za serikali za mitaa mwaka huu ili wawe katika maamuzi. 

Mwisho. 

Post a Comment

Previous Post Next Post