SINGIDA UNGANENI NA MASHABIKI WENGINE KATIKA MATUKIO MAKUBWA Y SIMBA - AHMED ALLY

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amewaomba Mashabiki wa Simba Mkoani Singida kushiriki katika matukio mbalimbali yanayohusu klabu yao ili waweke uhusiano mzuri na Mashabiki wengine.



Amewaambia ya kuwa ni vyema waweke mipango sawa ili matawi yaliyopo Mkoani Singida yatambulike kama yalivyo matawi mengine ambayo yanatoka Mikoa mingine inayofanya safari kuishangilia timu yao.

Hayo ameyaongea leo akiwa na Mashabiki wa Simba  Mkoani hapa akimtaka Mwenyekiti wa Simba Mkoa wa Singida wasimamie matawi yashiriki katika shughuli  mbali mbali za Simba.


"Wanasimba wa Singida msilale mnapilima alizeti na mpunga uko sawa basi mje katika majambo makubwa ya timu yenu," Ahmed

Akizungunzia juu ya mchezo wa kesho amesema kuwa ni mchezo mgumu ambao unahitaji nguvu na akili nyingi ili washinde mchezo huo.

"Mechi hii TUKIPATA Matokeo mazurii tutatengeneza Imani na ujasiri na morali katika kuelekea tarehe 20 michezo hii miwili ndio yanakutengeneza ubingwa wetu wa Ligi Kuu naamini inawezekana," amesema.

Amesema kuwa kwa Sasa wamebakiwa na ushiriki wa kombe moja la Ligi Kuu Tanzania bara ambapo tayari wameshachukua Ngao ya Jamii ambapo kombe hili ni miongoni mwa makombe matatu yaliyopo nchini Tanzania.

"Nafasi ya ubingwa bado iko wazi endapo tutatumia vizuri katika michezo hiyo basi tunaweza kuchukua ubingwa,"Ahmed Ally


Ahmed ametanabaisha ya kuwa wametolewa Michuano ya ligi ya mabingwa kwa hatua ambayo wameifikia sio kufeli bali wameweza kukaaa katika nafasi yao ya katika klabu bingwa Africa.

"Katika miaka mitano tumecheza Michuano hiyo ambapo kuna timu nne tumecheza nazo Hadi Sasa hazijarudi katika Michuano ya Klabu bingwa, Kaizer Chief, TP Mazembe, Wydad Casablanca, Orlando Pirates nao wamejaribu na tumecheza nao Hadi Sasa hatujui wako wapi," Ahmed.

Lakini ameongeza kuwa kutoka hatua wanayofikia kila wakati wanayouwezo wa kwenda hatua inayofuata.

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post