SHUSHENI BEI YA MAJI SHUWASA- MTATIRO

Na Sayi Mathias, Shinyanga


Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga(SHUWASA)  wametakiwa kushusha mara moja bei  za maji  kwenye Kata mbalimabli za Jimbo la Shinyanga  Vijijini, ili bei mpya ziwe sawa na zile za Shinyanga Mjini.




Rai hiyo imetolewa na  Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro wakati akiwa kwenye Mkutano wa hadhara kusikiliza na kutaua karo na changamoto za wananchi wa Shinyanga Vijijini ambapo ameielekeza Mamlaka hiyo kushusha  bei za maji haraka iwezekanavyo.       

 Mwakilishi wa Mkurugezi wa Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola amekiri kupokea maelekezo hayo na  kusema kuwa wataanza kuyatekeleza mara moja.



Kuanzia sasa Bei za Maji kata za Didia, Tinde na Iselamagazi zenye jumla ya wakazi takribani 55,000 itakuwa shilingi 1,490 kwa wanaotumia uniti 1 - 5 kwa mwezi na shilingi 1,700+ kwa wanaotumia uniti 6+ tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo kwa  miaka mitatu mfululizo wamekuwa wakilipa bili za maji kwa uniti moja shilingi 2,525 na hakukuwa na suluhu kwa sababu SHUWASA na EWURA walikuwa wanavutana katika kufanya uamuzi husika. 



Mtatiro anaendelea na ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika tarafa zote 6 za Wilaya ya Shinyanga.     

 

Post a Comment

Previous Post Next Post